Sura: AL-AARAAF 

Aya : 65

۞وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Na kwa (kabila la) Aadi (tulimtuma) ndugu yao Hudi akasema: Enyi watu wangu, muabuduni Allah; hamna nyinyi Mola mwingine Mlezi zaidi yake. Basi hamuogopi (adhabu yake)?



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 66

قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي سَفَاهَةٖ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Mamwinyi ambao wamekufuru katika watu wake wakasema: Kwa hakika, sisi tunakuona umo katika upumbavu na kwa hakika kabisa tunakudhania (tuna wasiwasi nawe) kuwa wewe ni miongoni mwa waongo



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 67

قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي سَفَاهَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

(Mtume Nuhu) Akasema: Enyi watu wangu, mimi sina upumbavu wowote, lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 68

أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنَا۠ لَكُمۡ نَاصِحٌ أَمِينٌ

Ninakufikishieni ujumbe wa Mola wangu, na mimi kwenu ni mtoaji nasaha, muaminifu sana



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 69

أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ قَوۡمِ نُوحٖ وَزَادَكُمۡ فِي ٱلۡخَلۡقِ بَصۜۡطَةٗۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Hivi mmestaajabu kwa kukufikieni ukumbusho kutoka kwa Mola wenu Mlezi kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni? Na kumbukeni alivyokufanyeni makhalifa (warithi) baada ya watu wa Nuhu, na akakuongezeeni umbo kubwa. Basi zikumbukeni neema za Allah ili mfaulu



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 70

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِنَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَحۡدَهُۥ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Wakasema: Hivi umetujia kwa ajili ya kuwa tumuabudu Allah peke yake na tuache (Miungu) wote ambao baba zetu walikuwa wanawaabudu? Basi tuletee (hayo) unayotuahidi ukiwa unasema kweli



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 71

قَالَ قَدۡ وَقَعَ عَلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ رِجۡسٞ وَغَضَبٌۖ أَتُجَٰدِلُونَنِي فِيٓ أَسۡمَآءٖ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّا نَزَّلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٖۚ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Akasema: Hakika, imekwisha kufikeni adhabu na ghadhabu kutoka kwa Mola wenu. Hivi mnajadiliana nami katika majina mliyoyataja (mliyoyazusha) nyinyi na baba zenu na Allah hakuteremsha dalili kuhusiana nayo? Basi ngojeeni na mimi pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kungojea



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 72

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَقَطَعۡنَا دَابِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ وَمَا كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ

Basi tukamuokoa yeye na wale waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mzizi wa wale waliozikadhibisha Aya zetu na hawakuwa waumini



Sura: HUUD 

Aya : 50

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۖ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُفۡتَرُونَ

Na (tulimpeleka kwa kabila la) Aadi ndugu yao Hudi. Akawaambia: Enyi watu wangu! Mwabuduni Allah; Hamna nyinyi Mungu mwingine zaidi yake. Na nyinyi hakuna mnachoabudu ispokuwa wazushi (waongo) tu



Sura: HUUD 

Aya : 51

يَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ أَجۡرًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱلَّذِي فَطَرَنِيٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Enyi watu wangu, siwaombeni ujira wowote (katika daawa yangu kwenu) hakika sivingine ujira wangu unatoka kwa yule tu aliyeniumba: hivi basi hamfahamu?



Sura: HUUD 

Aya : 52

وَيَٰقَوۡمِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا وَيَزِدۡكُمۡ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمۡ وَلَا تَتَوَلَّوۡاْ مُجۡرِمِينَ

Na enyi watu wangu! Ombeni msamaha kwa Mola wenu, kisha rudini kwake, atayatuma mawingu yatakayotiririsha kwenu mvua, na atawazidishieni nguvu kuongezea nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa Waovu



Sura: HUUD 

Aya : 53

قَالُواْ يَٰهُودُ مَا جِئۡتَنَا بِبَيِّنَةٖ وَمَا نَحۡنُ بِتَارِكِيٓ ءَالِهَتِنَا عَن قَوۡلِكَ وَمَا نَحۡنُ لَكَ بِمُؤۡمِنِينَ

Wakasema: Ewe Hudi! Hujatujia na dalili yoyote (itakayotubainishia ukweli wa madai yako), na sisi hatuwezi kuiacha Miungu yetu kwa kauli yako tu, na sisi kwako si wenye kukuamini



Sura: HUUD 

Aya : 54

إِن نَّقُولُ إِلَّا ٱعۡتَرَىٰكَ بَعۡضُ ءَالِهَتِنَا بِسُوٓءٖۗ قَالَ إِنِّيٓ أُشۡهِدُ ٱللَّهَ وَٱشۡهَدُوٓاْ أَنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ

Hatuna cha kusema ispokuwa baadhi ya Miungu yetu imekutia balaa (uwendawazimu). (Hudi) akasema: Hakika mimi namshuhudisha Allah, na shuhudieni kwamba mimi niko mbali na vyote mnavyovishirikisha na (Allah)



Sura: HUUD 

Aya : 55

مِن دُونِهِۦۖ فَكِيدُونِي جَمِيعٗا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ

Kinyume chake. Basi nyote nifanyieni vitimbi kisha msinipe muhula (muda wowote wakunisubiria)



Sura: HUUD 

Aya : 56

إِنِّي تَوَكَّلۡتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّي وَرَبِّكُمۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذُۢ بِنَاصِيَتِهَآۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Hakika mimi nimemtegemea Allah, Mola wangu mlezi na Mola wenu mlezi. Hakuna mnyama (kiumbe) yeyote ispokuwa yeye (Allah) amezishika nywele zake za utosi. Bila shaka Mola wangu mlezi yupo katika njia iliyonyooka



Sura: HUUD 

Aya : 57

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُم مَّآ أُرۡسِلۡتُ بِهِۦٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَيَسۡتَخۡلِفُ رَبِّي قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّونَهُۥ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَفِيظٞ

Na kama mtakengeuka, basi kwa hakika nimeshawafikishia kile nilichotumwa kwenu, na Mola wangu mlezi atawaleta watu wengine baada yenu, na nyinyi hamtamdhuru Yeye chochote. Hakika Mola wangu mlezi ni mwenye kukihifadhi kila kitu



Sura: HUUD 

Aya : 58

وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا هُودٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَنَجَّيۡنَٰهُم مِّنۡ عَذَابٍ غَلِيظٖ

Na ilipofika amri yetu, tulimuokoa Hudi na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na tukawaokoa katika adhabu ngumu



Sura: HUUD 

Aya : 59

وَتِلۡكَ عَادٞۖ جَحَدُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ وَعَصَوۡاْ رُسُلَهُۥ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٖ

Na (zile ni athari za kabila la) Aaadi. Walikanusha Aya za Mola wao mlezi, na wakamuasi Mtume wake (Huud), na wakafuata amri za kila aliye hodari sana mkaidi



Sura: HUUD 

Aya : 60

وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ عَادٗا كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّعَادٖ قَوۡمِ هُودٖ

Na wakafuatiliziwa laana hapa duniani na Siku ya Kiyama. Eleweni! Hakika (watu) Aadi wamemkufuru Mola wao mlezi. Eleweni! Maangamizi yawafike (kabila la) Aadi, watu wa Huud



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 123

كَذَّبَتۡ عَادٌ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Kina A’d waliwakanusha Mitume



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 124

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamumchi Allah?



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 125

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 126

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Basi mcheni Allah, na nitiini mimi



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 127

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 128

أَتَبۡنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةٗ تَعۡبَثُونَ

Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 129

وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمۡ تَخۡلُدُونَ

Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 130

وَإِذَا بَطَشۡتُم بَطَشۡتُمۡ جَبَّارِينَ

Na mnapotumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 131

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Basi mcheni Allah, na nitiini



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 132

وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِيٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعۡلَمُونَ

Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 133

أَمَدَّكُم بِأَنۡعَٰمٖ وَبَنِينَ

Amekupeni wanyama wa kufuga na watoto