Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 200

فَإِذَا قَضَيۡتُم مَّنَٰسِكَكُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَذِكۡرِكُمۡ ءَابَآءَكُمۡ أَوۡ أَشَدَّ ذِكۡرٗاۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَمَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖ

Mtakapomaliza ibada zenu, basi mtajeni Allah, kama mnavyowataja baba zenu au zaidi. Na miongoni mwa watu wapo wanaosema: “Ewe Mola wetu tupe katika dunia, na hawatakuwa na fungu lolote Akhera



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 201

وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Na baadhi yao wapo wanaosema: Ewe Mola wetu, tupe katika dunia wema, na Akhera wema na utukinge na adhabu ya Moto



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 202

أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ نَصِيبٞ مِّمَّا كَسَبُواْۚ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Hao wanalo fungu katika waliyoyachuma. Na Allah ni Mwepesi wa kuhesabu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 14

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٰتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ وَٱلۡحَرۡثِۗ ذَٰلِكَ مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ

Watu wamepambiwa kupenda kutamani wanawake na watoto wanaume na marundo mengi ya dhahabu na fedha na farasi wanaofunzwa na wanyama wafugwao na mashamba. Hizo ni starehe za maisha ya duniani, na mafikio mazuri yapo kwa Allah tu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 77

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَشۡتَرُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَأَيۡمَٰنِهِمۡ ثَمَنٗا قَلِيلًا أُوْلَـٰٓئِكَ لَا خَلَٰقَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيۡهِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Hakika, wale wanaouza ahadi ya Allah na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawatakuwa na fungu (la kheri yoyote) Akhera, na Allah hatazungumza nao (mazungumzo ya huruma) na hatawaangalia (kwa huruma) Siku ya Kiama na hatowatakasa (kwa kusamehe dhambi zao) na watapata adhabu kali mno



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 85

وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na yeyote atakayetaka dini isiyokuwa Uislamu, hatakubaliwa na Akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 145

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ كِتَٰبٗا مُّؤَجَّلٗاۗ وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلۡأٓخِرَةِ نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَاۚ وَسَنَجۡزِي ٱلشَّـٰكِرِينَ

Na nafsi yoyote haifi isipokuwa kwa idhini ya Allah tu ikiwa ni jambo lililoandikwa (na lenye) muda maalum. Na yeyote anayetaka malipo ya duniani tunampa humo, na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa huko. Na tutawalipa wenye kushukuru



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 176

وَلَا يَحۡزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡكُفۡرِۚ إِنَّهُمۡ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۚ يُرِيدُ ٱللَّهُ أَلَّا يَجۡعَلَ لَهُمۡ حَظّٗا فِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Wala wasikuhuzunishe ambao wanaharakisha kukimbilia ukafiri, hakika hao hawatamdhuru Allah, chochote anataka asiwawekee fungu lolote Akhera, nao watakuwa na adhabu kubwa mno



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 198

لَٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ رَبَّهُمۡ لَهُمۡ جَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا نُزُلٗا مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۗ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّلۡأَبۡرَارِ

Lakini wale wamchao Mola wao, wana Pepo zenye kutiririka chini yake mito na watabaki humo, ni makaribisho kutoka kwa Allah, na kilicho kwa Allah ni bora mno kwa wafanyao mema



Sura: ANNISAI 

Aya : 77

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ قِيلَ لَهُمۡ كُفُّوٓاْ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقِتَالُ إِذَا فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ يَخۡشَوۡنَ ٱلنَّاسَ كَخَشۡيَةِ ٱللَّهِ أَوۡ أَشَدَّ خَشۡيَةٗۚ وَقَالُواْ رَبَّنَا لِمَ كَتَبۡتَ عَلَيۡنَا ٱلۡقِتَالَ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖۗ قُلۡ مَتَٰعُ ٱلدُّنۡيَا قَلِيلٞ وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّمَنِ ٱتَّقَىٰ وَلَا تُظۡلَمُونَ فَتِيلًا

Je, hukuwaona wale ambao wakiambiwa: Zuieni mikono yenu (acheni vita) na simamisheni Swala na toeni Zaka? Basi walipoandikiwa (walipowajibishiwa) vita mara kundi miongoni mwao wanawaogopa watu kama wanavyomuogopa Allah au zaidi (ya kumuogopa Allah). Na wamesema: Kwanini umetufaradhishia kupigana? Ingekuwa bora kutuchelewesha mpaka muda wa karibu (ili tufe kifo cha kawaida). Sema (uwaambie): Raha ya duniani ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye Ucha Mungu, na hamtadhulumiwa (jambo lolote hata kama ni dogo kama) uzi wa kokwa ya tende



Sura: ANNISAI 

Aya : 134

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ ثَوَابُ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا

Anayetaka malipo ya dunia, basi kwa Allah yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kuona



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 32

وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا لَعِبٞ وَلَهۡوٞۖ وَلَلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na maisha ya duniani si chochote isipokuwa tu ni mchezo na pumbao. Na kwa yakini kabisa, nyumba ya Akhera ndio bora zaidi kwa wanaomcha Allah. Je, hamtumii akili?



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 147

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡۚ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na ambao wamekadhibisha Aya zetu na mkutano wa Akhera amali zao zimeporomoka (zimeharibika). Hawatalipwa isipokuwa yale tu waliyokuwa wakiyatenda



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 169

فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٞ وَرِثُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَأۡخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا ٱلۡأَدۡنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغۡفَرُ لَنَا وَإِن يَأۡتِهِمۡ عَرَضٞ مِّثۡلُهُۥ يَأۡخُذُوهُۚ أَلَمۡ يُؤۡخَذۡ عَلَيۡهِم مِّيثَٰقُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن لَّا يَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّ وَدَرَسُواْ مَا فِيهِۗ وَٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Basi kikafuatia baada yao kizazi kibaya kilichorithi kitabu (Taurati); wanashika anasa za haya maisha duni sana (ya duniani), na huku wanasema: Tutasamehewa (tu, acha tule maisha). Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wanaichukua. Hivi haikuchukuliwa kwao ahadi nzito ya kitabu kwamba, wasimsemee Allah isipokuwa haki tu na ilhali wamesoma yaliyomo kwenye kitabu hicho? Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanaomcha Allah. Hivi hamtumii akili?



Sura: ATTAUBA 

Aya : 38

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَا لَكُمۡ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلۡتُمۡ إِلَى ٱلۡأَرۡضِۚ أَرَضِيتُم بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ فَمَا مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ

Enyi mlioamini, mna nini wakati mnapoambiwa: Nendeni haraka katika Njia ya Allah (Jihadi), mnajitia uzito katika ardhi (kwa kubaki majumbani na kuwa wazito katika kuitikia wito wa Jihadi)? Je, mmeyaridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Basi hazikuwa starehe za maisha ya dunia ukizilinganisha na za Akhera isipokuwa ni chache mno



Sura: YUNUS 

Aya : 62

أَلَآ إِنَّ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهِ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Zindukeni: Hakika, Mawalii (wapenzi) wa Allah hawana hofu (yoyote) na hawahuzuniki



Sura: YUNUS 

Aya : 63

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

(Mawalii wa Allah ni) Ambao wameamini na wakawa wacha Mungu



Sura: YUNUS 

Aya : 64

لَهُمُ ٱلۡبُشۡرَىٰ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ لَا تَبۡدِيلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Wana bishara (habari njema) katika maisha ya duniani (kwa kupata wanachokipenda) na Akhera (kwa kuingia Peponi). Hakuna kubadilishwa kwa maneno ya Allah. Hayo ndio mafanikio makubwa



Sura: HUUD 

Aya : 15

مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيۡهِمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ فِيهَا وَهُمۡ فِيهَا لَا يُبۡخَسُونَ

Wale wanaotaka (katika matendo yao wanayofanya wapate) maisha ya kidunia na mapambo yake (kama dhahabu, fedha, watoto nafasi, wanawake nk), tutawalipa (thawabu hizo) kikamilifu hapa duniani na hawatapunguziwa chochote



Sura: HUUD 

Aya : 16

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَيۡسَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا ٱلنَّارُۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hao ndio wale ambao Akhera hawana chochote isipokuwa Moto tu, na yataharibika matendo yao yote na ni batili yote waliyokuwa wakiyatenda



Sura: YUSUF 

Aya : 57

وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

Na kwa hakika kabisa, malipo ya Akhera ni bora zaidi kwa walioamini na wakawa wanamcha Allah



Sura: YUSUF 

Aya : 109

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na hatukutuma kabla yako isipokuwa (Mitume) wanaume tunaowafunulia (tunaowashushia Wahyi) miongoni mwa watu wa mijini. Je, hivi hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Na hakika, nyumba ya Akhera ni bora kwa wanaomcha Allah. Basi hamtumii akili?



Sura: AR-RA’D 

Aya : 26

ٱللَّهُ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ وَفَرِحُواْ بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا مَتَٰعٞ

Allah humkunjulia riziki amtakaye, na huibana. Na (watu wa Makkah) wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo



Sura: AR-RA’D 

Aya : 34

لَّهُمۡ عَذَابٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَقُّۖ وَمَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٖ

(Hao makafiri) Wana adhabu katika maisha ya dunia, na adhabu ya Akhera ni nzito mno. Na wala hawatakuwa na wa kuwahami na (adhabu ya) Allah



Sura: IBRAHIM 

Aya : 27

يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّـٰلِمِينَۚ وَيَفۡعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ

Allah anawathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti[1] katika maisha ya dunia (kaburini)[2] na katika Akhera. Na Allah huwapoteza madhalimu. Na Allah anafanya analolitaka


1- - Neno madhubuti na imara ni Lailaha illa llah na kila neno la haki na kweli


2- - Wakati watakapokuwa wanaulizwa na Malaika wawili kuhusu Mola wao, Dini yao na Mtume wao?


Sura: ANNAHLI 

Aya : 22

إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Mungu wenu ni Mungu mmoja; Basi walewasioiamini Akhera nyoyo zao zinapinga tu ilhali wao wanafanya kiburi (kuikubali haki.)



Sura: ANNAHLI 

Aya : 41

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na wale waliohama kwa ajili ya Allah baada ya kudhulumiwa, bila shaka tutawakalisha katika dunia kwa wema na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti wangekuwa wanajua!



Sura: ANNAHLI 

Aya : 96

مَا عِندَكُمۡ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٖۗ وَلَنَجۡزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓاْ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Allah ndivyo vibakiavyo; na kwa yakini sisi tutawapa waliosubiri ujira wao sawa na matendo mazuri waliyokuwa wakiyatenda



Sura: ANNAHLI 

Aya : 97

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Atakayefanya mema, mwana-mume au mwanamke, ilhali ni muumini, basi kwa hakika tutampa maisha mema na kwa yakini tutawapa ujira wao kwa uzuri zaidi kuliko yale waliokuwa wakiyatenda



Sura: ANNAHLI 

Aya : 107

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Hayo ni kwa sababu wame-yapenda zaidi maisha ya dunia kuliko Akhera, na kwa hakika Allah hawaongozi watu makafiri