Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 1

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi ambaye ameumba



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 2

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ

Amemuumba binaadamu kwa tone la damu



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 3

ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ

Soma! Na Mola wako Mlezi ni Mkarimu kushinda wote!