Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 125

وَإِذۡ جَعَلۡنَا ٱلۡبَيۡتَ مَثَابَةٗ لِّلنَّاسِ وَأَمۡنٗا وَٱتَّخِذُواْ مِن مَّقَامِ إِبۡرَٰهِـۧمَ مُصَلّٗىۖ وَعَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيۡتِيَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلۡعَٰكِفِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ

Na (kumbuka) tulipoifanya Kaaba sehemu ya watu kurejea na mahali pa amani, nafanyeni mahali aliposimama Ibrahimu mahali pakuswali. Na tukawaagiza Ibrahimu na Ismaili, (kuwa) itwaharisheni Nyumba yangu kwa ajili ya wanaofanya twawafu na wanaokaa itikafu na wanaorukuu na kusujudu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 126

وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا بَلَدًا ءَامِنٗا وَٱرۡزُقۡ أَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُم بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُۥ قَلِيلٗا ثُمَّ أَضۡطَرُّهُۥٓ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلنَّارِۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na (kumbuka) aliposema Ibrahimu: “Ewe Mola wangu, ufanye mji huu (wa Makkah) uwe wa amani, na waruzuku watu wake katika matunda; yule aliye muamini Allah miongoni mwao na kuamini Siku ya Mwisho. (Allah) akasema: Na mwenye kukufuru nitamstarehesha kidogo kisha nitamswaga kwenda kwenye adhabu ya moto, na hatima mbaya mno ni hiyo



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 127

وَإِذۡ يَرۡفَعُ إِبۡرَٰهِـۧمُ ٱلۡقَوَاعِدَ مِنَ ٱلۡبَيۡتِ وَإِسۡمَٰعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلۡ مِنَّآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na (kumbuka wakati) Ibrahimu na Ismaili wanainua misingi ya Kaaba (wakisema): “Ewe Mola wetu, tukubalie. Hakika, wewe ndiye msikivu, mjuzi sana



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 128

رَبَّنَا وَٱجۡعَلۡنَا مُسۡلِمَيۡنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَآ أُمَّةٗ مُّسۡلِمَةٗ لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبۡ عَلَيۡنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Ewe Mola wetu, tufanye sisi tuwe watiifu kwako, na katika kizazi chetu wawe umma mtiifu kwako. Na tuelekeze ibada zetu na pokea toba zetu. Hakika wewe tu ndiye mwingi wa kupokea toba mwingi wa rehema



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 129

رَبَّنَا وَٱبۡعَثۡ فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُزَكِّيهِمۡۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Ewe Mola wetu, na wapelekee Mtume miongoni mwao, atakayewasomea Aya zako na kuwafundisha kitabu na hekima na kuwatakasa. Hakika wewe tu ndiye mwenye nguvu kubwa mwingi wa hekima



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 133

أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ حَضَرَ يَعۡقُوبَ ٱلۡمَوۡتُ إِذۡ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعۡبُدُونَ مِنۢ بَعۡدِيۖ قَالُواْ نَعۡبُدُ إِلَٰهَكَ وَإِلَٰهَ ءَابَآئِكَ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ إِلَٰهٗا وَٰحِدٗا وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ

Je, mlikuwepo wakati Yakubu yalipomfika mauti, pale alipowaambia watoto wake: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mola wako na (ambaye ndiye) Mola wa baba zako Ibrahimu na Ismaili na Is-haka, Mola Mmoja, na sisi tumejisalimisha kwake tu



Sura: ANNISAI 

Aya : 163

۞إِنَّآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ كَمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ نُوحٖ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيۡمَٰنَۚ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا

Hakika, sisi tumekufunulia (Wahyi) kama tulivyomfunulia (Wahyi) Nuhu na Manabii (wengine) baada yake. Na tumemfunulia (Wahyi) Ibrahimu na Ismail na Isihaka na Yakubu na kizazi (chake) na Issa na Ayubu na Yunus na Haruna na Sulaimani. Na tulimpa Daudi Zaburi



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 86

وَإِسۡمَٰعِيلَ وَٱلۡيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطٗاۚ وَكُلّٗا فَضَّلۡنَا عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na Ismaili na Alyasaa na Yunus na Lutwi. Na wote (hao) tumewafanya bora kuliko walimwengu (wengine wa zama zao)



Sura: MARYAM 

Aya : 54

وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ إِسۡمَٰعِيلَۚ إِنَّهُۥ كَانَ صَادِقَ ٱلۡوَعۡدِ وَكَانَ رَسُولٗا نَّبِيّٗا

Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii



Sura: MARYAM 

Aya : 55

وَكَانَ يَأۡمُرُ أَهۡلَهُۥ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِۦ مَرۡضِيّٗا

Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, na alikuwa ni mwenye kuridhiwa mbele ya Mola wake Mlezi



Sura: AL-ANBIYAA 

Aya : 85

وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِدۡرِيسَ وَذَا ٱلۡكِفۡلِۖ كُلّٞ مِّنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli, wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri



Sura: SWAAD 

Aya : 48

وَٱذۡكُرۡ إِسۡمَٰعِيلَ وَٱلۡيَسَعَ وَذَا ٱلۡكِفۡلِۖ وَكُلّٞ مِّنَ ٱلۡأَخۡيَارِ

Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora