Sura: AL-ANKABUUT 

Aya : 32

قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطٗاۚ قَالُواْ نَحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَن فِيهَاۖ لَنُنَجِّيَنَّهُۥ وَأَهۡلَهُۥٓ إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Akasema: Hakika humo yumo Lutwi. Wao wakasema: Sisi tunajua zaidi nani yumo humo. Hapana shaka tutamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe aliye miongoni mwa wataokaa nyuma



Sura: AL-ANKABUUT 

Aya : 33

وَلَمَّآ أَن جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗاۖ وَقَالُواْ لَا تَخَفۡ وَلَا تَحۡزَنۡ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهۡلَكَ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Na wajumbe wetu walipo mfikia Lutwi, alihuzunika kwa ajili yao, na moyo uliona dhiki kwa ajili yao. Wakasema: Usiogope, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, ila mkeo aliye miongoni mwa wataokaa nyuma



Sura: AL-ANKABUUT 

Aya : 34

إِنَّا مُنزِلُونَ عَلَىٰٓ أَهۡلِ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Kwa yakini sisi tutawateremshia watu wa mji huu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya uchafu wanao ufanya



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 133

وَإِنَّ لُوطٗا لَّمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Na hakika Lutwi bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 134

إِذۡ نَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ

Tulipo mwokoa yeye na watu wake wote,



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 135

إِلَّا عَجُوزٗا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ

Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 136

ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ

Kisha tukawaangamiza wale wengineo



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 137

وَإِنَّكُمۡ لَتَمُرُّونَ عَلَيۡهِم مُّصۡبِحِينَ

Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 138

وَبِٱلَّيۡلِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?



Sura: AL-QAMAR

Aya : 33

كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطِۭ بِٱلنُّذُرِ

Wamekadhibisha Watu wa Luutwi Mitume waonyaji



Sura: AL-QAMAR

Aya : 34

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ

Hakika Sisi Tumewapelekea Upepo Uliyo Na Mchanga Ispokua Watu Wa Luutwi Waliyomuamini Tuliwaokoa Wakati Wa Theluthi Ya Mwisho Ya Usiku



Sura: AL-QAMAR

Aya : 35

نِّعۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَن شَكَرَ

Neema kutoka Kwetu, hivyo ndivyo Tunavyomlipa ambaye ameshukuru



Sura: AL-QAMAR

Aya : 36

وَلَقَدۡ أَنذَرَهُم بَطۡشَتَنَا فَتَمَارَوۡاْ بِٱلنُّذُرِ

Na Hakika Aliwaonya Kuhusiana Na Adhabu Yetu Wakatia Shaka Na Maonyo Hayo



Sura: AL-QAMAR

Aya : 37

وَلَقَدۡ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيۡفِهِۦ فَطَمَسۡنَآ أَعۡيُنَهُمۡ فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ

Na kwa yakini walimshawishi awape wageni wake, basi Tukawapofoa macho yao. Basi onjeni adhabu Yangu na maonyo Yangu



Sura: AL-QAMAR

Aya : 38

وَلَقَدۡ صَبَّحَهُم بُكۡرَةً عَذَابٞ مُّسۡتَقِرّٞ

Hakika Iliwafika Wao Adhabu Yenye Kudumu Asubuhi Mapema



Sura: AL-QAMAR

Aya : 39

فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ

Basi Onjeni Adhabu Yangu na Maonyo