Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 143

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَٰكُمۡ أُمَّةٗ وَسَطٗا لِّتَكُونُواْ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ وَيَكُونَ ٱلرَّسُولُ عَلَيۡكُمۡ شَهِيدٗاۗ وَمَا جَعَلۡنَا ٱلۡقِبۡلَةَ ٱلَّتِي كُنتَ عَلَيۡهَآ إِلَّا لِنَعۡلَمَ مَن يَتَّبِعُ ٱلرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِۚ وَإِن كَانَتۡ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَٰنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Na kama hivyo tumekufanyeni umma bora ili muwe mashahidi kwa watu, na Mtume awe shahidi kwenu. Na hatukukiweka Kibla ulichokuwa unaelekea isipokuwa tu tumjue nani anamfuata Mtume na nani atakayerejea nyuma. Ilivyo ni kwamba hilo ni zito sana isipokuwa kwa wale ambao Allah amewaongoza. Na Allah hapotezi imani zenu. Kwa hakika kabisa Allah ni Mpole mno kwa watu, Mwenye huruma sana



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 20

فَإِنۡ حَآجُّوكَ فَقُلۡ أَسۡلَمۡتُ وَجۡهِيَ لِلَّهِ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡأُمِّيِّـۧنَ ءَأَسۡلَمۡتُمۡۚ فَإِنۡ أَسۡلَمُواْ فَقَدِ ٱهۡتَدَواْۖ وَّإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Na kama watakuletea hoja (yoyote), basi sema: Nimeukabidhi uso wangu (nimejisalimisha) kwa Allah; mimi na wale walionifuata. Na waambie waliopewa kitabu na wasio na elimu kwamba: Je, mmesilimu (Mmejisalimisha kwa Allah)? Kama wamesilimu basi hakika wameongoka, na kama wakikataa, basi wajibu wako ni kufikisha tu. Na Allah anawaona mno waja



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 164

لَقَدۡ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذۡ بَعَثَ فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡ أَنفُسِهِمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ

kwa hakika Allah amewaneemesha Waumini pale alipomtuma kwao Mtume anayetokana na wao wenyewe, anawasomea Aya zake, anawatakasa na anawafundisha kitabu na hekima japokuwa kabla ya hapo walikuwa katika uovu wa wazi



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 67

۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ بَلِّغۡ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَۖ وَإِن لَّمۡ تَفۡعَلۡ فَمَا بَلَّغۡتَ رِسَالَتَهُۥۚ وَٱللَّهُ يَعۡصِمُكَ مِنَ ٱلنَّاسِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Ewe Mtume, fikisha uliyotere-mshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na usipofanya (hivyo) basi (utakuwa) hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda dhidi ya watu. Hakika, Allah hawaongozi (njia ya sawa) watu makafiri



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 92

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَٱحۡذَرُواْۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na mtiini Allah na mtiini Mtume, na jihadharini (na dhambi). Na mkikengeuka basi jueni ya kuwa jukumu la Mtume wetu ni kufikisha ujumbe wenye kufafanua



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 99

مَّا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا تَكۡتُمُونَ

Si juu ya Mtume isipokuwa kufikisha ujumbe tu. Na Allah anajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 14

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيّٗا فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَهُوَ يُطۡعِمُ وَلَا يُطۡعَمُۗ قُلۡ إِنِّيٓ أُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَسۡلَمَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Hivi nimfanye asiyekuwa Allah mwandani (Allah ambaye ni) Muumba wa mbingu na ardhi, na yeye ndiye analisha na halishwi? Sema: Hakika, mimi nimeamrishwa kuwa Muislamu wa kwanza (muumini wa kwanza wa haya ninayowaambia), na wewe kamwe usiwe katika washirikina



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 51

وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na waonye kwayo (Qur’ani) wale wanao ogopa kukusanywa kwa Mola wao wakiwa hawana msimamizi wala muombezi isipokuwa yeye (Allah), ili wamche Allah



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 52

وَلَا تَطۡرُدِ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ مَا عَلَيۡكَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَمَا مِنۡ حِسَابِكَ عَلَيۡهِم مِّن شَيۡءٖ فَتَطۡرُدَهُمۡ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na usiwafukuze wale wanaomuabudu Mola wao asubuhi na jioni, wakitaka radhi za Allah (kwa ibada zao hizo). Si jukumu lako kuwalipa chochote, na wao hawana jukumu la kukulipa chochote hadi iwe sababu ya kuwafukuza. Basi (ukifanya hivyo) utakuwa miongoni mwa madhalimu (wanaodhulumu nafsi zao kwa kufanya yasiyomridhisha Allah)



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 106

ٱتَّبِعۡ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Fuata yale yote uliyoletewa Wahyi kutoka kwa Mola wako. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu, na wapuuze washirikina[1]


1- - Hukumu ya Aya hii imefutwa na Aya 5 ya Sura Attauba (9).


Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 107

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشۡرَكُواْۗ وَمَا جَعَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظٗاۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٖ

Na lau kama Allah angetaka wasingeshirikisha. Na hatukukufanya Mlinzi wao, na wewe sio msimamizi wao



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 157

ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلرَّسُولَ ٱلنَّبِيَّ ٱلۡأُمِّيَّ ٱلَّذِي يَجِدُونَهُۥ مَكۡتُوبًا عِندَهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ يَأۡمُرُهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَىٰهُمۡ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡخَبَـٰٓئِثَ وَيَضَعُ عَنۡهُمۡ إِصۡرَهُمۡ وَٱلۡأَغۡلَٰلَ ٱلَّتِي كَانَتۡ عَلَيۡهِمۡۚ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِهِۦ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَٱتَّبَعُواْ ٱلنُّورَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ مَعَهُۥٓ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Ambao wanamfuata Mtume, Nabii, hasomi kilichoandikwa, ambaye kwao wanamkuta amean-dikwa katika Taurati na Injili, anawaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vilivyo vizuri, na anawaharamishia vilivyo vibaya, na anawaondoshea mazito yao (sheria zao ngumu) na makongwa (minyororo ya dhambi) waliyokuwa nayo. Basi wale waliomuamini (Mtume huyo) na wakamheshimu na wakamsaidia na wakaifuata nuru aliyoteremshiwa, hao tu ndio waliofanikiwa



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 184

أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ

Hivi hawatafakari? Huyu mwen-zao (Mtume Muhammad) hana chembe ya wazimu! Hakuwa yeye isipokuwa tu ni Muonyaji dhahiri



Sura: AN-FAL 

Aya : 65

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ حَرِّضِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَى ٱلۡقِتَالِۚ إِن يَكُن مِّنكُمۡ عِشۡرُونَ صَٰبِرُونَ يَغۡلِبُواْ مِاْئَتَيۡنِۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّاْئَةٞ يَغۡلِبُوٓاْ أَلۡفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Ewe Nabii, wahimize Waumini kupigana (dhidi ya makafiri na maadui wa Uislamu). Kati yenu wakiwepo (wapiganaji) ishirini wenye uvumilivu watawashinda (makafiri) mia mbili. Na kati yenu wakiwepo (wapiganaji) mia (moja) watawashinda makafiri elfu moja, kwasababu wao (makafiri) ni watu wasiofahamu (mantiki ya vita na wanapigana bila ya weledi)



Sura: ATTAUBA 

Aya : 73

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ جَٰهِدِ ٱلۡكُفَّارَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱغۡلُظۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Ewe Nabii, pambana na makafiri na wanafiki (kwa mbinu za aina zote) na uwe mkali kwao. Na makazi yao ni Jahanamu, na huo ni mwisho mbaya sana



Sura: ATTAUBA 

Aya : 103

خُذۡ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡ صَدَقَةٗ تُطَهِّرُهُمۡ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٞ لَّهُمۡۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Chukua sadaka (Zaka) kutoka katika mali zao (waumini ili) uwasafishe na uwatakase kwazo na waombee rehema. Hakika dua yako ni (sababu ya) utuvu kwao. Na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua



Sura: ATTAUBA 

Aya : 113

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن يَسۡتَغۡفِرُواْ لِلۡمُشۡرِكِينَ وَلَوۡ كَانُوٓاْ أُوْلِي قُرۡبَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ

Haiwi (haifai) kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina (makafiri), na hata kama watakuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kuwa hao ni watu wa Motoni



Sura: YUNUS 

Aya : 104

قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Sema: Enyi watu, ikiwa nyinyi mna shaka na (usahihi wa) dini yangu, basi mimi siabudu wale mnaowaabudu badala ya Allah. Na lakini ninamuabudu Allah ambaye anakufisheni, na nimeamrishwa kuwa miongoni mwa waumini



Sura: YUNUS 

Aya : 105

وَأَنۡ أَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفٗا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na (pia nimeamrishwa) kwamba: Elekeza uso wako katika dini[1] hali ya kumtakasa (Allah), na usiwe miongoni mwa washirikina


1- - Umetajwa uso hapa kwa sababu uso ndio unaofanya mwili wote ufuate. Maana ni kwamba, jikite na jielekeze katika dini kwa kufuata maelekezo ya Allah na Mtume wake kwa ukamilifu.


Sura: YUNUS 

Aya : 106

وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na usiombe (usiabudu) chochote badala ya Allah ambacho hakikunufaishi na hakikudhuru. Basi kama ukifanya hivyo, hakika wewe wakati huo utakuwa miongoni mwa madhalimu (wanaozidhulumu nafsi zao)



Sura: YUNUS 

Aya : 109

وَٱتَّبِعۡ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَٱصۡبِرۡ حَتَّىٰ يَحۡكُمَ ٱللَّهُۚ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Na fuata yale yanayofunuliwa kwako, na kuwa na subira hadi Allah ahukumu. Na yeye (Allah) ni Bora zaidi ya wanaohukumu



Sura: HUUD 

Aya : 2

أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ

(Kwamba) Msiabudu chochote ispokuwa Allah tu. Hakika mimi ninatoka kwake (nikiwa) Muonyaji na Mwenye kutoa habari njema



Sura: HUUD 

Aya : 112

فَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطۡغَوۡاْۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Basi, simama imara kama ulivyo amrishwa, na wale waliotubu pamoja na wewe, na msichupe mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo



Sura: HUUD 

Aya : 113

وَلَا تَرۡكَنُوٓاْ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

Wala msiwategemee wale walio dhulumu, na ikasababisha ukakuguseni Moto. na nyinyi hamna walinzi (wengine) badala ya Allah, kisha hamtanusuriwa



Sura: HUUD 

Aya : 114

وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّـٰكِرِينَ

Na simamisha swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku. Hakika mema huondoa maovu. Huo ni ukumbusho kwa wale wanaokumbuka



Sura: HUUD 

Aya : 115

وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na subiri (kuwa mvumilivu), kwani Allah hapotezi ujira wa wafanyao wema



Sura: AR-RA’D 

Aya : 40

وَإِن مَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ وَعَلَيۡنَا ٱلۡحِسَابُ

Na iwapo tutakuonesha baadhi ya (adhabu) tulizowaahidi au tukakufisha kabla yake (kabla ya kuwaadhibu), haikuwa jukumu lako wewe isipokuwa ni kufikisha ujumbe na juu yetu ni hesabu



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 89

وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ

Na sema: Hakika mimi ni muonyaji mwenye kubainisha



Sura: ANNAHLI 

Aya : 82

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na endapo watakengeuka basi hakika huna jukumu isipokuwa kufikisha (ujumbe) waziwazi tu



Sura: ANNAHLI 

Aya : 125

ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Waite (walinganie watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako mlezi yeye anamjua zaidi aliyepotea katika njia yake, na yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka