Sura: AL-IMRAN 

Aya : 33

۞إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰٓ ءَادَمَ وَنُوحٗا وَءَالَ إِبۡرَٰهِيمَ وَءَالَ عِمۡرَٰنَ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Hakika, Allah amemteua Adamu na Nuhu na familia ya Ibrahimu na familia ya Imrani kati ya walimwengu (wengine wa wakati wao)



Sura: ANNISAI 

Aya : 163

۞إِنَّآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ كَمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ نُوحٖ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيۡمَٰنَۚ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا

Hakika, sisi tumekufunulia (Wahyi) kama tulivyomfunulia (Wahyi) Nuhu na Manabii (wengine) baada yake. Na tumemfunulia (Wahyi) Ibrahimu na Ismail na Isihaka na Yakubu na kizazi (chake) na Issa na Ayubu na Yunus na Haruna na Sulaimani. Na tulimpa Daudi Zaburi



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 84

وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ كُلًّا هَدَيۡنَاۚ وَنُوحًا هَدَيۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَٰرُونَۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na tulimtunuku (Mtume Ibrahimu) Isihaka na Yakubu. Wote tuliwaongoa. Na Nuhu tulimuongoa kabla (yao). Na katika kizazi chake tulimongoa Daudi na Suleimani na Ayubu na Yusufu na Mussa na Haruna. Na kama hivyo tunawalipa wafanyao mazuri



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 59

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Kwa hakika kabisa, tulimpeleka Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu, muabuduni Allah (tu). Nyinyi hamna Mola mwingine zaidi yake. Hakika, mimi nakuhofieni (kupata) adhabu ya siku kubwa sana



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 60

قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Kundi la mamwinyi katika watu wake lilisema kuwa: Hakika, sisi tunakuona umo katika upotevu uliodhahiri sana



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 61

قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي ضَلَٰلَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

(Mtume Nuhu) Akasema: Enyi watu wangu, mimi sina upotevu wowote, lakini mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa wali-mwengu wote



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 62

أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمۡ وَأَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Ninakufikishieni ujumbe wa Mola wangu Mlezi na ninakupeni nasaha, na ninajua kwa Allah (mambo) msiyoyajua



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 63

أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡ وَلِتَتَّقُواْ وَلَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Hivi mnastaajabu kwamba, umekufikieni ukumbusho kutoka kwa Mola wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu, ili akuonyeni na ili muwe wacha Mungu na ili mpate rehema?



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 64

فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمًا عَمِينَ

Basi wakamkadhibisha na tukamuokoa yeye na wale waliokuwa pamoja naye katika jahazi, na tukawazamisha baharini wale waliozikadhibisha aya zetu. Bila shaka, hao walikuwa watu vipofu (wana nyoyo)



Sura: YUNUS 

Aya : 71

۞وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ

Na wasomee habari za (Mtume) Nuhu wakati alipowaambia watu wake kuwa: “Enyi watu wangu, ikiwa mnachukizwa na kuishi kwangu (na nyinyi) na kukumbusha kwangu Aya za Allah, basi mimi nimemtegemea Allah tu. Basi amueni jambo lenu nyinyi na washirika (Miungu) wenu, kisha jambo lenu lisiwe la kificho, kisha pitisheni hukumu kwangu na msinicheleweshe



Sura: YUNUS 

Aya : 72

فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَمَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

Basi mkikengeuka, mimi sikukuombeni ujira wowote. Ujira wangu haupo (popote) isipokuwa kwa Allah tu, na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu”



Sura: YUNUS 

Aya : 73

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ خَلَـٰٓئِفَ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Basi (watu wake) wakamka-dhibisha (wakampinga Mtume Nuhu), tukamuokoa yeye na waliokuwepo pamoja naye katika mashua, na tukawafanya warithi (wa nafasi za walioangamizwa) na tukawazamisha baharini wale waliozikadhibisha Aya zetu. Basi angalia namna ulivyokuwa mwisho wa walio onywa



Sura: HUUD 

Aya : 25

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ

Na kwa hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake (akawaambia watu wake kuwa) hakika mimi kwenu ni muonyaji ninaye bainisha



Sura: HUUD 

Aya : 26

أَن لَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ أَلِيمٖ

(Kwamba) musimuabudu yeyote ispokuwa Allah kwa hakika mimi ninaogopea kwenu adhabu ya siku yenye kuumiza mno



Sura: HUUD 

Aya : 27

فَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرٗا مِّثۡلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمۡ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ ٱلرَّأۡيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلِۭ بَلۡ نَظُنُّكُمۡ كَٰذِبِينَ

Wakasema waheshimiwa ambao wamekufuru katika watu wake: Wewe hatukuoni (chochote) ispokuwa tu ni mtu mfano wetu (sio Malaika) na hatuoni wafuasi wako ispokuwa tu ni wale ambao ni wanyonge wetu wenye mawazo duni, na hatuwaoni kuwa mnaubora wowote kwetu bali tuna hakika kuwa ni waongo



Sura: HUUD 

Aya : 28

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي رَحۡمَةٗ مِّنۡ عِندِهِۦ فَعُمِّيَتۡ عَلَيۡكُمۡ أَنُلۡزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمۡ لَهَا كَٰرِهُونَ

Akasema enyi jamaa zangu hivi mwaonaje nikiwa nina hoja kutoka kwa Mola wangu mlezi na amenipa rehema kutoka kwake na ikafichwa kwenu, hivi tuwalazimishe kukubali na ilhali nyinyi mnaichukia?



Sura: HUUD 

Aya : 29

وَيَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مَالًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْۚ إِنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَلَٰكِنِّيٓ أَرَىٰكُمۡ قَوۡمٗا تَجۡهَلُونَ

Na enyi jamaa zangu siwaombi mali (malipo kama ujira wa kazi ya kuwafikishia daawa) hakuna wakunilipa ispokuwa Allah tu, nami si mwenye kuwafukuza wale walioamini (kwa unyonge wao), kwa hakika wao watakutana na Mola wao mlezi lakini mimi ninakuoneni ni watu wajinga



Sura: HUUD 

Aya : 30

وَيَٰقَوۡمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِن طَرَدتُّهُمۡۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Na enyi jama zangu ninani atakaeninusuru kutokana na (adhabu ya) Allah iwapo nitawafukuza? Hivi hamuonyeki?



Sura: HUUD 

Aya : 31

وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّي مَلَكٞ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزۡدَرِيٓ أَعۡيُنُكُمۡ لَن يُؤۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيۡرًاۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا فِيٓ أَنفُسِهِمۡ إِنِّيٓ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na sisemi kuwa nina hazina za Allah na siwaambii kuwa mimi ninajua ghaibu na siwaambii (katika daawa yangu) kwamba mimi ni Malaika, na sisemi kuhusu wale yanawadharau macho yenu kuwa Allah hatawapa kheri yeyote. Allah ni Mjuzi zaidi wa yaliyo katika nafsi zao, (ikiwa nitayafanya hayo) kwa hakika kabisa nitakuwa miongoni mwa madhalimu



Sura: HUUD 

Aya : 32

قَالُواْ يَٰنُوحُ قَدۡ جَٰدَلۡتَنَا فَأَكۡثَرۡتَ جِدَٰلَنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Walisema ewe Nuhu kwa hakika umejadiliana nasisi na umezidisha mijadala yako kwetu, basi tuletee kile unachotukamia nacho kama kweli ni katika wasemao kweli



Sura: HUUD 

Aya : 33

قَالَ إِنَّمَا يَأۡتِيكُم بِهِ ٱللَّهُ إِن شَآءَ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ

(Nuhu) akasema: Hakika sivingine Allah ndiye atawaleteeni akitaka wala nyinyi si wenye kumshinda



Sura: HUUD 

Aya : 34

وَلَا يَنفَعُكُمۡ نُصۡحِيٓ إِنۡ أَرَدتُّ أَنۡ أَنصَحَ لَكُمۡ إِن كَانَ ٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يُغۡوِيَكُمۡۚ هُوَ رَبُّكُمۡ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Nasaha zangu hazitawafaa (chochote) iwapo Allah akitaka awaache mpotee, yeye tu ndiye Mola wenu mlezi na kwake tu mtarejeshwa



Sura: HUUD 

Aya : 35

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ إِنِ ٱفۡتَرَيۡتُهُۥ فَعَلَيَّ إِجۡرَامِي وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُجۡرِمُونَ

Au wanasema kuwa (kauli hii Nuhu) ameizusha tu, sema kama itakuwa nimeizusha basi kosa la uzushi ni langu peke yangu, na mimi niko mbali na yote mnayoyafanya



Sura: HUUD 

Aya : 36

وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُۥ لَن يُؤۡمِنَ مِن قَوۡمِكَ إِلَّا مَن قَدۡ ءَامَنَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Na akapewa wah-yi Nuhu ya kwamba hataamini katika watu wako yeyote ispokuwa tu yule aliyekwisha amini, hivyo basi usihuzunike kutokana na yale waliyokuwa wakiyatenda



Sura: HUUD 

Aya : 37

وَٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡيُنِنَا وَوَحۡيِنَا وَلَا تُخَٰطِبۡنِي فِي ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ

Na unda jahazi mbele ya macho yetu na na wah-yi wetu. Na usiniambie lolote kuhusu wale waliodhulumu (nafsi zao), kwa yakini wao watazamishwa



Sura: HUUD 

Aya : 38

وَيَصۡنَعُ ٱلۡفُلۡكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيۡهِ مَلَأٞ مِّن قَوۡمِهِۦ سَخِرُواْ مِنۡهُۚ قَالَ إِن تَسۡخَرُواْ مِنَّا فَإِنَّا نَسۡخَرُ مِنكُمۡ كَمَا تَسۡخَرُونَ

Na (Nuhu alianza) kuuunda jahazi; Na wakubwa wa watu wake kila walipopita pale walimdhihaki, (Nuhu) akasema: Ijapokuwa mnatudhihaki, hakika na sisi tutawadhihaki kama mnavyo-tudhihaki



Sura: HUUD 

Aya : 39

فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيۡهِ عَذَابٞ مُّقِيمٌ

Basi mtajua ni nani itakayemfika adhabu ya kumfedhehesha na itamteremkia adhabu yenye kudumu



Sura: HUUD 

Aya : 40

حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَمۡرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ قُلۡنَا ٱحۡمِلۡ فِيهَا مِن كُلّٖ زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَأَهۡلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيۡهِ ٱلۡقَوۡلُ وَمَنۡ ءَامَنَۚ وَمَآ ءَامَنَ مَعَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلٞ

Hadi ilipofika amri yetu (ya kuwaangamiza) na chemchem ya maji ikabubujika, tukamwambia (Nuhu): pakia humo (katika jahazi) kila mnyama pea moja jike na dume, na (pakia) ahali zako ispokuwa yule ambaye imepita hukumu na walioamini. Na hawakuamini pamoja na Nuhu ispokuwa wachache tu



Sura: HUUD 

Aya : 41

۞وَقَالَ ٱرۡكَبُواْ فِيهَا بِسۡمِ ٱللَّهِ مَجۡرٜىٰهَا وَمُرۡسَىٰهَآۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na akasema: Pandeni humo, kwa jina la Allah (Bismillah arrahmani arrahim) iwe kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu mlezi ni msamehevu sana mwenye kurehemu



Sura: HUUD 

Aya : 42

وَهِيَ تَجۡرِي بِهِمۡ فِي مَوۡجٖ كَٱلۡجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ٱبۡنَهُۥ وَكَانَ فِي مَعۡزِلٖ يَٰبُنَيَّ ٱرۡكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Nayo ili kwenda nao katika mawimbi mfano wa milima. Na Nuhu alimwita mwanawe aliyekuwa mbali: ewe mwanangu panda pamoja na sisi na usiwe pamoja na makafiri