يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Enyi watu, muabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na (ameumba) waliokuwepo kabla yenu ili muwe Wacha Mungu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٌ
Enyi watu, kuleni vilivyomo katika ardhi vikiwa halali na vizuri. Na msifuate nyendo za shetani kwa sababu, bila ya shaka, yeye kwenu ni adui aliye wazi
وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا تُرۡجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na iogopeni siku ambayo mtarejeshwa kwa Allah, kisha kila mtu atalipwa kikamilifu aliyoyachuma, nao hawatadhulumiwa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَخَلَقَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا وَبَثَّ مِنۡهُمَا رِجَالٗا كَثِيرٗا وَنِسَآءٗۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِي تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلۡأَرۡحَامَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيۡكُمۡ رَقِيبٗا
Enyi watu, mcheni Mola wenu Mlezi Ambaye amekuumbeni kutokana na nafsi moja tu na ameumba kutoka kwenye nafsi hiyo mke wake (Hawaa), na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume wengi na wanawake (wengi), na mcheni Allah Ambaye mnaombana kupitia yeye, na (ogopeni kukata) udugu. Hakika, Allah amekuwa Mwenye kukufuatilieni kwa karibu sana
۞إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُكُمۡ أَن تُؤَدُّواْ ٱلۡأَمَٰنَٰتِ إِلَىٰٓ أَهۡلِهَا وَإِذَا حَكَمۡتُم بَيۡنَ ٱلنَّاسِ أَن تَحۡكُمُواْ بِٱلۡعَدۡلِۚ إِنَّ ٱللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا
Hakika, Allah anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe, na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika, mazuri mno anayokuwaidhini Allah ni hayo. HakikaAllah ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلۡحَقِّ مِن رَّبِّكُمۡ فَـَٔامِنُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Enyi watu, hakika amekujieni Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, iwe kheri kwenu. Na mkikufuru basi hakika ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Allah ni Mjuzi sana, Mwenye hekima
هَٰذَا بَلَٰغٞ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُواْ بِهِۦ وَلِيَعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ وَلِيَذَّكَّرَ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ
Hii (Qur’ani) ni ufikisho (wa ujumbe) kwa watu, na ili waonywe na ili wapate kujua kuwa, uhakika ni kwamba Yeye (Allah) ni Muabudiwa mmoja tu, na ili wenye akili wapate kuonyeka
وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٖ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا
Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’ani kwa kila mfano. Lakini watu wengi wanakataa isipo kuwa kukanusha tu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡۚ إِنَّ زَلۡزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَيۡءٌ عَظِيمٞ
Enyi watu, mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Kiyama ni jambo kubwa mno
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡ وَٱخۡشَوۡاْ يَوۡمٗا لَّا يَجۡزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِۦ وَلَا مَوۡلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِۦ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Allah ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala asikudanganyeni juu ya Allah mdanganyifu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ هَلۡ مِنۡ خَٰلِقٍ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ
Enyi watu, kumbukeni neema za Allah kwenu. Ati yupo Muumba mwingine asiyekuwa Allah anayekupeni riziki kutoka mbinguni na ardhini? Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa ila Yeye tu. Basi vipi mnageuzwa (mnapotoshwa)?
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ
Enyi watu! Hakika ahadi ya Allah ni ya kweli. Basi yasiku-danganyeni maisha ya dunia, wala mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Allah
إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمۡ عَدُوّٞ فَٱتَّخِذُوهُ عَدُوًّاۚ إِنَّمَا يَدۡعُواْ حِزۡبَهُۥ لِيَكُونُواْ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ
Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni