Sura: AL-AARAAF 

Aya : 131

فَإِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡحَسَنَةُ قَالُواْ لَنَا هَٰذِهِۦۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَطَّيَّرُواْ بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓۗ أَلَآ إِنَّمَا طَـٰٓئِرُهُمۡ عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Basi linapowajia jambo zuri (mvua na rutuba) husema: Hili ni stahiki yetu, na likiwapata jambo baya (ukame na magonjwa) wanaamini kuwa ni nuksi ya Musa na walioko pamoja naye! Eleweni kwamba, mikosi yao inatoka kwa Allah na lakini wengi wao hawajui



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 132

وَقَالُواْ مَهۡمَا تَأۡتِنَا بِهِۦ مِنۡ ءَايَةٖ لِّتَسۡحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحۡنُ لَكَ بِمُؤۡمِنِينَ

Na wakasema: Muujiza wowote utakaotuletea ili uturoge, basi sisi hatutakuamini



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 133

فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلطُّوفَانَ وَٱلۡجَرَادَ وَٱلۡقُمَّلَ وَٱلضَّفَادِعَ وَٱلدَّمَ ءَايَٰتٖ مُّفَصَّلَٰتٖ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ

Basi tuliwapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu ikiwa ni miujiza iliyowekwa wazi wakafanya kiburi na wakawa watu waovu



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 134

وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ

Na adhabu ilipowashukia walisema: (Ewe Musa) Tuombee Mola wako Mlezi zile ahadi alizokuahidi. Kwa hakika kabisa, ukituondolea (hii) adhabu tutakuamini na tutawaachia Wana wa Israili waondoke pamoja nawe



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 135

فَلَمَّا كَشَفۡنَا عَنۡهُمُ ٱلرِّجۡزَ إِلَىٰٓ أَجَلٍ هُم بَٰلِغُوهُ إِذَا هُمۡ يَنكُثُونَ

Basi tulipowaondolea adhabu mpaka muda wao watakaoufikia, ghafla wao wakawa wanavunja ahadi



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 136

فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ فَأَغۡرَقۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ

Basi tuliwaadhibu tukawaza-misha baharini kwa sababu walikadhibisha Aya zetu na wali-kuwa wakizipuuza



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 137

وَأَوۡرَثۡنَا ٱلۡقَوۡمَ ٱلَّذِينَ كَانُواْ يُسۡتَضۡعَفُونَ مَشَٰرِقَ ٱلۡأَرۡضِ وَمَغَٰرِبَهَا ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۖ وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلۡحُسۡنَىٰ عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُواْۖ وَدَمَّرۡنَا مَا كَانَ يَصۡنَعُ فِرۡعَوۡنُ وَقَوۡمُهُۥ وَمَا كَانُواْ يَعۡرِشُونَ

Na tuliwarithisha watu waliokuwa wananyanyaswa mashariki ya ardhi (Shamu) na magharibi yake ambayo tumeibariki. Na neno zuri la Mola wako limetimia kwa Wana wa Israili kwa sababu walivumilia na tuliyaangamiza yote aliyotengeneza Firauni na watu wake, na (majumba ya kifahari) waliyokuwa wakiyajenga



Sura: AN-FAL 

Aya : 54

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ فَأَهۡلَكۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَۚ وَكُلّٞ كَانُواْ ظَٰلِمِينَ

(Hali ya Makafiri wa Kikureshi) Ni kama desturi ya watu wa Firauni na waliokuwepo kabla yao; walizipinga Aya za Mola wao Mlezi, basi tuliwaangamiza kwasababu ya dhambi zao na tuliwazamisha majini watu wa Firauni. Na wote walikuwa madhalimu



Sura: YUNUS 

Aya : 75

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ

Kisha tukamtuma Musa na Haruna baada ya hao kwenda kwa Firauni na mamwinyi wake (wakiwa na) Aya zetu. Basi wakafanya kiburi na wakawa watu wakosefu



Sura: YUNUS 

Aya : 76

فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰذَا لَسِحۡرٞ مُّبِينٞ

Basi ilipowajia haki kutoka kwetu walisema: “Bila shaka, huu hasa ni uchawi ulio dhahiri sana”



Sura: YUNUS 

Aya : 77

قَالَ مُوسَىٰٓ أَتَقُولُونَ لِلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَكُمۡۖ أَسِحۡرٌ هَٰذَا وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّـٰحِرُونَ

Akasema Musa: Hivi, mnasema kuhusu haki ilipokujieni kwamba, huu ni uchawi? Na wachawi hawafaulu



Sura: YUNUS 

Aya : 78

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَلۡفِتَنَا عَمَّا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا نَحۡنُ لَكُمَا بِمُؤۡمِنِينَ

Wakasema: “Hivi, umetujia ili utuondoe katika yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ukubwa uwe wenu wawili nyie katika ardhi? Na sisi kamwe hatutakuaminini”



Sura: YUNUS 

Aya : 79

وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ ٱئۡتُونِي بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ

Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mahiri sana



Sura: YUNUS 

Aya : 80

فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلۡقُواْ مَآ أَنتُم مُّلۡقُونَ

Basi wachawi walipofika, Musa aliwaambia: Tupeni (chini) mnavyotaka kuvitupa (chini)



Sura: YUNUS 

Aya : 81

فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئۡتُم بِهِ ٱلسِّحۡرُۖ إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبۡطِلُهُۥٓ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُصۡلِحُ عَمَلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Basi (wachawi) walipotupa, Musa akasema: “Hiki mlicholeta ni uchawi. Hakika, Allah ataubatilisha. Hakika, Allah hastawishi vitendo vya waharibifu”



Sura: YUNUS 

Aya : 82

وَيُحِقُّ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Na Allah anahakikisha haki inashinda kwa maneno yake, na hata kama waovu watachukia



Sura: YUNUS 

Aya : 83

فَمَآ ءَامَنَ لِمُوسَىٰٓ إِلَّا ذُرِّيَّةٞ مِّن قَوۡمِهِۦ عَلَىٰ خَوۡفٖ مِّن فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِمۡ أَن يَفۡتِنَهُمۡۚ وَإِنَّ فِرۡعَوۡنَ لَعَالٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ

Basi hakuna aliyemuamini Musa (pamoja na dalili na hoja zote alizowaonesha) isipokuwa vijana wachache katika kaumu yake huku wakiwa na hofu (ya kumuogopa) Firauni na mamwinyi wao wasiwatese. Na hakika kabisa, Firauni alikuwa mwenye kujikweza ardhini, na kwa yakini kabisa yeye (Firauni) alikuwa miongoni mwa waliokiuka mipaka (katika kufanya uovu)



Sura: YUNUS 

Aya : 84

وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰقَوۡمِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ فَعَلَيۡهِ تَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّسۡلِمِينَ

Na Musa alisema: Enyi watu wangu, kama kweli nyinyi mmemuamini Allah, basi mtegemeeni yeye tu, kama nyinyi mkiwa Waislamu (kweli)



Sura: YUNUS 

Aya : 85

فَقَالُواْ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَا رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Basi wakasema: “Allah tu tunamtegemea. Ewe Mola wetu Mlezi, usitufanye mtihani kwa watu madhalimu”



Sura: YUNUS 

Aya : 86

وَنَجِّنَا بِرَحۡمَتِكَ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na utuokoe kwa rehema zako dhidi ya watu makafiri



Sura: YUNUS 

Aya : 87

وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّءَا لِقَوۡمِكُمَا بِمِصۡرَ بُيُوتٗا وَٱجۡعَلُواْ بُيُوتَكُمۡ قِبۡلَةٗ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na tulimpa Wahyi Musa na ndugu yake (Haruna) ya kuwa: Wawekeeni makazi (wajengeeni nyumba) watu wenu (katika mji wa) Misri na zifanyeni nyumba zenu ziwe na mahala pa ibada na simamisheni Swala na wape bishara Waumini



Sura: YUNUS 

Aya : 88

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَآ إِنَّكَ ءَاتَيۡتَ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَأَهُۥ زِينَةٗ وَأَمۡوَٰلٗا فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّواْ عَن سَبِيلِكَۖ رَبَّنَا ٱطۡمِسۡ عَلَىٰٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ وَٱشۡدُدۡ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُواْ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ

Na Musa alisema: “(Ewe) Mola wetu Mlezi, bila shaka umempa Firauni na mamwinyi wake mapambo na mali nyingi katika maisha ya duniani (na hawakukushukuru). (Ewe) Mola wetu Mlezi, (umewapa hivyo vyote na wanavitumia) ili kuwapoteza (watu) wasiifuate njia yako. (Ewe) Mola wetu Mlezi, zifute Mali zao na mioyo yao ifanye kuwa migumu ili wasiamini hadi waione adhabu iumizayo mno”



Sura: YUNUS 

Aya : 89

قَالَ قَدۡ أُجِيبَت دَّعۡوَتُكُمَا فَٱسۡتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَآنِّ سَبِيلَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

(Allah) Akasema: Hakika maombi yenu yamekubaliwa. Basi simameni imara na katu msifuate njia ya wale wasiojua (wasiokuwa na elimu)



Sura: YUNUS 

Aya : 90

۞وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ وَجُنُودُهُۥ بَغۡيٗا وَعَدۡوًاۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَدۡرَكَهُ ٱلۡغَرَقُ قَالَ ءَامَنتُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱلَّذِيٓ ءَامَنَتۡ بِهِۦ بَنُوٓاْ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَأَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

Na tuliwavusha Wana wa Israeli baharini. Basi Firauni na majeshi yake waliwafuata kwa nia ovu na uadui hadi (Firauni) ilipomfikia gharika, alisema: Nimeamini kwamba, hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa tu yule ambaye Wana wa Israili wamemuamini, na mimi ni miongoni mwa Waislamu



Sura: YUNUS 

Aya : 91

ءَآلۡـَٰٔنَ وَقَدۡ عَصَيۡتَ قَبۡلُ وَكُنتَ مِنَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Je, hivi sasa (ndio umeamini) na ilhali kwa hakika uliasi hapo kabla na ukawa miongoni mwa waharibifu?



Sura: YUNUS 

Aya : 92

فَٱلۡيَوۡمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنۡ خَلۡفَكَ ءَايَةٗۚ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنۡ ءَايَٰتِنَا لَغَٰفِلُونَ

Basi leo tunauopoa mwili wako ili uwe ishara (na fundisho) kwa walioko nyuma yako (kwamba wewe sio Mungu). Na hakika kabisa, watu wengi ni wenye kughafilika na aya zetu



Sura: HUUD 

Aya : 97

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ فِرۡعَوۡنَۖ وَمَآ أَمۡرُ فِرۡعَوۡنَ بِرَشِيدٖ

Kwenda kwa firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao walifuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa na busara



Sura: HUUD 

Aya : 98

يَقۡدُمُ قَوۡمَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَأَوۡرَدَهُمُ ٱلنَّارَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡوِرۡدُ ٱلۡمَوۡرُودُ

Siku ya Kiyama (Firauni) atawatangulia watu wake na atawaingiza Motoni (kama alivyokuwa akiwatangulia duniani). Na ubaya ulioje huo wataoingia!



Sura: HUUD 

Aya : 99

وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِۦ لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ بِئۡسَ ٱلرِّفۡدُ ٱلۡمَرۡفُودُ

Na wamefuatishiwa laana hapa duniani na Siku ya Kiyama. Ni mabaya yalioje watakayo pewa!



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 101

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ تِسۡعَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ فَسۡـَٔلۡ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ إِذۡ جَآءَهُمۡ فَقَالَ لَهُۥ فِرۡعَوۡنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰمُوسَىٰ مَسۡحُورٗا

Na kwa yakini tulimpa Mussa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Mussa umerogwa!