Sura: AL-MAIDA 

Aya : 83

وَإِذَا سَمِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعۡيُنَهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ مِمَّا عَرَفُواْ مِنَ ٱلۡحَقِّۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ

Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanabubujika machozi kwasababu ya haki waliyoitambua. Wanasema: Ewe Mola wetu Mlezi, tumeamini; basi tuandike (tuwe) pamoja na wanaoshuhudia (Uungu wako, upekee wako na kuabudiwa kwako)



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 84

وَمَا لَنَا لَا نُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡحَقِّ وَنَطۡمَعُ أَن يُدۡخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na kwanini tusimuamini Allah na haki iliyotujia (Qur’an) Na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na watu wema?



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 104

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُواْ حَسۡبُنَا مَا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَآؤُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَهۡتَدُونَ

Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allah, na kwa Mtume, wanasema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, (wanafuata waliyoyakuta kwa baba zao) hata kama baba zao hao hawajui kitu na hawana muongozo?



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 7

وَلَوۡ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ كِتَٰبٗا فِي قِرۡطَاسٖ فَلَمَسُوهُ بِأَيۡدِيهِمۡ لَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na lau kama tungekuteremshia kitabu (kikiwa) katika (mfumo wa) karatasi na wakakigusa kwa mikono yao, hakika kabisa waliokufuru wangesema: Hayakuwa haya isipokuwa ni uchawi wa wazi



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 30

وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ قَالَ أَلَيۡسَ هَٰذَا بِٱلۡحَقِّۚ قَالُواْ بَلَىٰ وَرَبِّنَاۚ قَالَ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

Na lau kama utawaona wakati watakaposimamishwa kwa Mola wao atasema Allah na kuwaambia): Hivi hili (la kufufuliwa) sio kweli? Watasema: Tunaapa kwa Mola wetu (kwamba ni kweli). (Allah) Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayapinga



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 92

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَاۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَهُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na hii (Qur’ani) ni kitabu tulichokiteremsha, kilochobarikiwa, kinachosadikisha (kitabu) kilichoko mbele yake na (tumekiteremsha) ili uwaonye (kwacho watu wa mji wa) Mama wa Miji (Makkah) na walioko (katika miji iliyopo) pembezoni mwake[1]. Na wale wanaoamini Akhera (kuwa ipo) wanakiamini kitabu hicho, nao wanadumisha Swala zao


1- - Kinachokusudiwa hapa ni maeneo mengine ya dunia. Qur’ani imeteremka kwa ajili ya watu wote duniani. Rejea Aya ya 41 ya sura Azzumar (39). Pia rejea Aya ya 51-52 ya Sura Alqalam (68).


Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 114

أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡتَغِي حَكَمٗا وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مُفَصَّلٗاۚ وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٞ مِّن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Hivi nitake hakimu (muamuzi) asiyekuwa Allah, na ilhali yeye ndiye aliyekuteremshieni kitabu kikiwa kimefafanuliwa? Na wale tuliowapa kitabu wanajua kwamba kimetereshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki. Kwa hiyo usiwe miongoni mwa wenye shaka kabisa



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 155

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na hii (Qur’ani) ni kitabu tulichokiteremsha, chenye baraka. Basi kifuateni na mcheni Allah ili mpate kushushiwa rehema



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 2

كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

(Hii Qur’ani ni) Kitabu ulichoteremshiwa. Basi kusiwe na uzito wowote ndani ya kifua chako juu yake (usikose raha katika kukiamini na kukitangaza). (Umeteremshiwa kitabu hiki) Ili kwacho uwaonye (watu) na (ili kiwe) ukumbusho kwa waumini



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 170

وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ

Na ambao wanakishika vilivyo kitabu (bila ya kukipuuza au kukifanyia mzaha) na wakadumisha Swala, hakika sisi hatupotezi ujira wa watengenezao (mambo ya kumridhisha Allah)



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 196

إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّـٰلِحِينَ

Hakika, mlinzi wangu ni Allah ambaye ameteremsha kitabu (Qur’ani), naye ndiye anawalinda waja wema



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 203

وَإِذَا لَمۡ تَأۡتِهِم بِـَٔايَةٖ قَالُواْ لَوۡلَا ٱجۡتَبَيۡتَهَاۚ قُلۡ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ مِن رَّبِّيۚ هَٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Na usipowaletea Aya (zile wanazozitaka wao au muujiza wanaoutaka) wanasema: Kwa nini usiubuni (usilete wa kutengeneza)? Sema (uwaambie kuwa): Ukweli ni kwamba, mimi nafuata kile kinachofunuliwa kwangu (Wahyi) kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Hii (Qur’ani) ni mwangaza kutoka kwa Mola wenu Mlezi na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 204

وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na wakati inasomwa Qur’ani isikilizeni na nyamazeni ili mpate kupewa rehema[1]


1- - Aya hii ina mafunzo makubwa kwa Muislamu. 1) Kuiheshimu Qur’ani kwa kuisikiliza na kukaa kimya. 2) Muislamu anapata rehema kwa kutekeleza agizo la kusikiliza na kukaa kimya. 3) Kama kusikiliza tu na kukaa kimya Muislamu anapata rehema, hii inaonesha kwamba kuifanyia kazi Qur’ani na kutekeleza mafunzo yake kuna rehema zaidi. 4) Ni muhimu kwa Muislamu kuangalia mazingira ya kusoma Qur’ani. Kwa muktadha huu, si jambo jema na ni makuruhu kusoma Qur’ani au kuweka sauti ya Qu’ani katika mazingira ambayo sio rafiki kama kwenye mikusanyiko ya sokoni, dukani, ndani ya vyombo vya usafiri n.k.


Sura: AN-FAL 

Aya : 2

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Kwa hakika kabisa, Waumini (kamili) ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa Aya zake huwaongezea imani, na wanamtegemea Mola wao Mlezi tu



Sura: AN-FAL 

Aya : 31

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا قَالُواْ قَدۡ سَمِعۡنَا لَوۡ نَشَآءُ لَقُلۡنَا مِثۡلَ هَٰذَآ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na (Washirikina) wanaposomewa Aya zetu, husema: “Tumesikia; laiti tungetaka (nasi) tungesema kama hii (Qur’ani). Hii (Qur’an) si chochote ila ni ngano za watu wa kale tu”



Sura: ATTAUBA 

Aya : 124

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na inapoteremshwa Sura wapo miongoni mwao wanaosema (kwa kebehi): Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Basi ama wale walioamini imewazidishia Imani, nao wanafurahia



Sura: ATTAUBA 

Aya : 125

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَتۡهُمۡ رِجۡسًا إِلَىٰ رِجۡسِهِمۡ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ

Na ama wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi (ya unafiki), basi (Sura) imewazidishia uchafu (uovu) juu ya uchafu (uovu) wao; na wanakufa hali ya kuwa ni makafiri



Sura: ATTAUBA 

Aya : 127

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ نَّظَرَ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ هَلۡ يَرَىٰكُم مِّنۡ أَحَدٖ ثُمَّ ٱنصَرَفُواْۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Na ikiteremshwa Sura wanata-zamana (wanakonyezana) wao kwa wao, (kana kwamba wanasema): Je, kuna mtu yeyote anayekuoneni (mkiamua kuondoka kwa Mtume)? Kisha huondoka (kwa Mtume kwa kuogopa aibu). Allah amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu



Sura: YUNUS 

Aya : 15

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَاتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا ٱئۡتِ بِقُرۡءَانٍ غَيۡرِ هَٰذَآ أَوۡ بَدِّلۡهُۚ قُلۡ مَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلۡقَآيِٕ نَفۡسِيٓۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۖ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Na wakati wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji (wasioamini) kukutana nasi wana-sema: “lete Qur’ani (nyingine) isiyokuwa hii au ibadilishe. Sema: “Haiwezekani kwangu kuibadili kwa utashi wangu. Sifuati isipokuwa tu yanayofunuliwa kwangu. Hakika mimi naogopa adhabu ya Siku iliyo kubwa sana ikiwa nitamuasi Mola wangu Mlezi



Sura: YUNUS 

Aya : 16

قُل لَّوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوۡتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَدۡرَىٰكُم بِهِۦۖ فَقَدۡ لَبِثۡتُ فِيكُمۡ عُمُرٗا مِّن قَبۡلِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Sema: Lau kama Allah angetaka nisingekusomeeni (hii Qur’ani), na (Allah) asingekujulisheni (kuwa hiyo Qur’ani ni haki), kwa sababu bila ya shaka yoyote nimekaa nanyi umri mwingi kabla yake (kabla ya kuletewa hii Qur’ani na wala sikukuambieni kuwa mimi nimeleta Qur’ani). Je, hamtumii akili?



Sura: YUNUS 

Aya : 37

وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na haiwezekani Qur’ani hii kutungwa na yeyote kinyume na Allah, lakini (Qur’ani) ni usadikisho wa yote yaliyotangulia (katika vitabu na sheria za Manabii waliotangulia), na ni ufafanuzi wa kitabu (sheria za umma wa Muhammad) kisichokuwa na shaka kutoka kwa Mola mlezi wa walimwengu wote



Sura: YUNUS 

Aya : 38

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Au wanasema (kuwa Muhammad) ameitunga (hiyo Qur’ani)? Sema: Basi leteni sura moja tu mfano wake na waiteni muwawezao kuwaleta kinyume na Allah (wakusaidieni), kama nyinyi ni wa kweli (katika madai yenu)



Sura: YUNUS 

Aya : 94

فَإِن كُنتَ فِي شَكّٖ مِّمَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ فَسۡـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقۡرَءُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكَۚ لَقَدۡ جَآءَكَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Basi kama una shaka katika yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma kitabu (Taurati) kabla yako. Kwa yakini kabisa, haki imekwisha kukufikia kutoka kwa Mola wako Mlezi. Kwa hiyo, katu usiwe miongoni mwa watiao shaka



Sura: HUUD 

Aya : 1

الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ

Alif, laam, raa (hizi ni herufi za mkato na Allah ndiye anayejua maana yake). Hiki ni kitabu (ambacho) zimetengenezwa vyema Aya zake kisha zimefafanuliwa kutoka kwa aliye na Hekima, Mwenye habari nyingi



Sura: HUUD 

Aya : 13

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِعَشۡرِ سُوَرٖ مِّثۡلِهِۦ مُفۡتَرَيَٰتٖ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Au wanasema hii Qur’ani ameizua? Sema: Leteni Sura kumi zilizozushwa mfano wake na muiteni mtakayeweza (kumuita) badala ya Allah kama mkiwa wa kweli (katika madai yenu)



Sura: HUUD 

Aya : 14

فَإِلَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَآ أُنزِلَ بِعِلۡمِ ٱللَّهِ وَأَن لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ

Na kama hawakukujibuni hilo basi juweni kwamba, sivinginevyo (Qur’ani imeteremshwa kwa elimu ya Allah na hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Yeye tu je nyinyi mmesilimu?



Sura: HUUD 

Aya : 17

أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ وَيَتۡلُوهُ شَاهِدٞ مِّنۡهُ وَمِن قَبۡلِهِۦ كِتَٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامٗا وَرَحۡمَةًۚ أُوْلَـٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ مِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ فَٱلنَّارُ مَوۡعِدُهُۥۚ فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّنۡهُۚ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hivi yule aliye na hoja kutoka kwa Mola wake mlezi na akaifuata (hoja hiyo) shahidi kutoka kwake (Jibrili) na kabla yake palikuwepo kitabu (cha taurati kilichoteremshwa kwa Nabii) Musa juu yake amani, kikiwa ni kiongozi na rehema, hao wanaiamini Qur ani, na yeyote anaeikufuru miongoni mwa makundi, basi Moto ni mahali pake alipoahidiwa, basi usiwe katika shaka yoyote, hii Qur’ani ni haki kutoka kwa bwana wako, lakini watu wengi hawaamini



Sura: YUSUF 

Aya : 2

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Hakika, sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu ili mpate kuelewa



Sura: YUSUF 

Aya : 3

نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ

Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa (huu) Wahyi tuliokufunulia wa hii Qur’ani, na ingawa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua



Sura: YUSUF 

Aya : 111

لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Kwa hakika kabisa, katika simulizi zao (hao Mitume) kuna mazingatio kwa wenye akili. Haikuwa (hii Qur’an ni) maneno yanayozushwa lakini ni usadikisho (uthibitisho) wa (maandiko matakatifu) yaliyokuwepo kabla yake (Taurati na Injili) na ni ufafanuzi wa kila kitu na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini