Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 177

۞لَّيۡسَ ٱلۡبِرَّ أَن تُوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ قِبَلَ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلۡكِتَٰبِ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ وَءَاتَى ٱلۡمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ ذَوِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَٱلسَّآئِلِينَ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُوفُونَ بِعَهۡدِهِمۡ إِذَا عَٰهَدُواْۖ وَٱلصَّـٰبِرِينَ فِي ٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَحِينَ ٱلۡبَأۡسِۗ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُتَّقُونَ

Sio wema peke yake kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni (wa) wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Vitabu na Manabii, na wanatoa mali pamoja na kuwa wanaipenda wakawapa ndugu na mayatima na maskini na wasafiri na waombao na katika (kuwakomboa) watumwa, na wakawa wanasimamisha swala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na madhara na (katika) wakati wa vita. Hao ndio wa kweli na hao ndio wa mchao Allah



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 224

وَلَا تَجۡعَلُواْ ٱللَّهَ عُرۡضَةٗ لِّأَيۡمَٰنِكُمۡ أَن تَبَرُّواْ وَتَتَّقُواْ وَتُصۡلِحُواْ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Msimfanye Allah kinga ya viapo vyenu mkaacha kufanya wema na kumcha (Allah) na kufanya suluhu kati ya watu. Na Allah ni Mwingi wa kusikia, Mjuzi mno



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 277

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Hakika wale walioamini na kutenda vitendo vizuri na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, wanamalipo mema mbele ya Mola wao, na hawana hofu yoyote, na hawahuzuniki



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 57

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na ama walioamini na wakatenda mema, basi (Allah) atawalipa malipo yao kamili, na Allah hawapendi madhalimu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 92

لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ

Hamtaupata wema hadi mtoe katika mnavyovipenda. Na kitu chochote mtakachokitoa, hakika Allah anakijua sana



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 133

۞وَسَارِعُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ أُعِدَّتۡ لِلۡمُتَّقِينَ

Na ukimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi na Pepo (ambayo) upana wake ni mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wacha Mungu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 134

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي ٱلسَّرَّآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَٱلۡكَٰظِمِينَ ٱلۡغَيۡظَ وَٱلۡعَافِينَ عَنِ ٱلنَّاسِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

(Wacha Mungu) Ambao wanatoa (katika vile walivyopewa na Allah) katika hali ya wasaa na katika hali ya dhiki, na wenye kuzuia hasira (zao) na kusamehe watu (wanaowakosea). Na Allah anawapenda wafanyao mazuri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 135

وَٱلَّذِينَ إِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةً أَوۡ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ ذَكَرُواْ ٱللَّهَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ لِذُنُوبِهِمۡ وَمَن يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ إِلَّا ٱللَّهُ وَلَمۡ يُصِرُّواْ عَلَىٰ مَا فَعَلُواْ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Na ambao wafanyapo uovu (wamadhambi makubwa) au wakazidhulumu nafsi zao (kwa kufanya madhambi madogo) wanamkumbuka Allah na kuomba msamaha kwa dhambi zao (hizo) na hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Allah tu, na hawaendelei kufanya (madhambi) waliyoyafanya na ilhali wanajua



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 199

وَإِنَّ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَمَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِمۡ خَٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشۡتَرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Na kwa hakika katika Watu wa kitabu wapo wanaomuamini Allah hasa na kilichoteremshwa kwenu na kilichoteremshwa kwao, huku wakinyenyekea kwa Allah. Hawauzi Aya za Allah kwa thamani ndogo (ya dunia). Hao malipo yao yako kwa Mola wao mlezi, hakika Allah ni mwepesi mno wa kuhesabu



Sura: ANNISAI 

Aya : 124

وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَـٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا

Na yeyote anayefanya mema awe mwanaume au mwanamke na ilhali ni Muumini, basi hao wataingia Peponi na hawatadhulumiwa (jema lolote) hata kama liwe ujazo wa uwazi wa tundu ya kokwa ya tende



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 2

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُحِلُّواْ شَعَـٰٓئِرَ ٱللَّهِ وَلَا ٱلشَّهۡرَ ٱلۡحَرَامَ وَلَا ٱلۡهَدۡيَ وَلَا ٱلۡقَلَـٰٓئِدَ وَلَآ ءَآمِّينَ ٱلۡبَيۡتَ ٱلۡحَرَامَ يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّهِمۡ وَرِضۡوَٰنٗاۚ وَإِذَا حَلَلۡتُمۡ فَٱصۡطَادُواْۚ وَلَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شَنَـَٔانُ قَوۡمٍ أَن صَدُّوكُمۡ عَنِ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ أَن تَعۡتَدُواْۘ وَتَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Enyi mlioamini, msizivunjie heshima alama za (dini) ya Allah[1] wala Miezi Mitukufu[2] wala Hadiy[3] wala vigwe[4], wala wakusudiao Nyumba Takatifu[5] wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao. Na mkishatoka (katika Ibada ya Hija au Umrah) basi windeni (mkitaka kufanya hivyo). Na wala kule kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuieni kufika Msikiti Mtukufu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui (wa kuwaua na mfano wa hilo). Na saidianeni katika wema na ucha Mungu, na msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allah. Hakika, Allah ni Mkali sana wa kuadhibu


1- - Alama za dini ya Allah ni zile ibada kubwa kama Hija, Umra, Swala, Funga n.k.


2- - Miezi Mitukufu ni minne: Dhul-qaada, Dhulhija, Muharram na Rajab.


3- - Hadiyu ni wanyama wanaopelekwa Makka kwa kuchinjwa katika ibada ya Hija.


4- - Vigwe ni kamba za utambulisho anayofungwa mnyama shingoni ili kumtambulisha kuwa anapelekwa Makkah kwa kuchinjwa katika ibada ya Hija.


5- - Hawa ni wale Waislamu wanaokwenda Makka kwa makusudi ya kufanya ibada ya Hija au Umra.


Sura: AL-AARAAF 

Aya : 42

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na wale walioamini na wakatenda yaliyo mema hatutamkalifisha mtu yeyote (kufanya) isipokuwa tu aliwezalo. Hao ndio watu wa Peponi, wao humo watakaa milele



Sura: AN-FAL 

Aya : 1

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَنفَالِۖ قُلِ ٱلۡأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَصۡلِحُواْ ذَاتَ بَيۡنِكُمۡۖ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

(Ewe Nabii) Wanakuuliza kuhusu (utaratibu wa ugawaji wa) Ngawira. Sema: Ngawira ni za Allah na Mtume (wao ndio watoaji wa utaratibu wa mgao wake). Basi mcheni Allah (kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake) na tatueni migogoro baina yenu, na mtiini Allah na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini



Sura: ANNAHLI 

Aya : 97

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Atakayefanya mema, mwana-mume au mwanamke, ilhali ni muumini, basi kwa hakika tutampa maisha mema na kwa yakini tutawapa ujira wao kwa uzuri zaidi kuliko yale waliokuwa wakiyatenda



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 22

لَّا تَجۡعَلۡ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَقۡعُدَ مَذۡمُومٗا مَّخۡذُولٗا

Usimfanye mungu mwengine pamoja na Allah, usije ukawa wa kulaumiwa uliye tupika



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 23

۞وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنًاۚ إِمَّا يَبۡلُغَنَّ عِندَكَ ٱلۡكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوۡ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفّٖ وَلَا تَنۡهَرۡهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوۡلٗا كَرِيمٗا

Na Mola wako Mlezi ameam-risha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwa-tendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 24

وَٱخۡفِضۡ لَهُمَا جَنَاحَ ٱلذُّلِّ مِنَ ٱلرَّحۡمَةِ وَقُل رَّبِّ ٱرۡحَمۡهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرٗا

Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 25

رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمۡۚ إِن تَكُونُواْ صَٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلۡأَوَّـٰبِينَ غَفُورٗا

Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwasamehe wanao tubia kwake



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 26

وَءَاتِ ذَا ٱلۡقُرۡبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلۡمِسۡكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرۡ تَبۡذِيرًا

Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 27

إِنَّ ٱلۡمُبَذِّرِينَ كَانُوٓاْ إِخۡوَٰنَ ٱلشَّيَٰطِينِۖ وَكَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لِرَبِّهِۦ كَفُورٗا

Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashetani. Na Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 28

وَإِمَّا تُعۡرِضَنَّ عَنۡهُمُ ٱبۡتِغَآءَ رَحۡمَةٖ مِّن رَّبِّكَ تَرۡجُوهَا فَقُل لَّهُمۡ قَوۡلٗا مَّيۡسُورٗا

Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema nao maneno laini



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 29

وَلَا تَجۡعَلۡ يَدَكَ مَغۡلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبۡسُطۡهَا كُلَّ ٱلۡبَسۡطِ فَتَقۡعُدَ مَلُومٗا مَّحۡسُورًا

Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 30

إِنَّ رَبَّكَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرٗا

Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 31

وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُمۡ خَشۡيَةَ إِمۡلَٰقٖۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُهُمۡ وَإِيَّاكُمۡۚ إِنَّ قَتۡلَهُمۡ كَانَ خِطۡـٔٗا كَبِيرٗا

Wala msiwauwe watoto wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni hatia (kosa) kubwa sana



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 32

وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓۖ إِنَّهُۥ كَانَ فَٰحِشَةٗ وَسَآءَ سَبِيلٗا

Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 33

وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَمَن قُتِلَ مَظۡلُومٗا فَقَدۡ جَعَلۡنَا لِوَلِيِّهِۦ سُلۡطَٰنٗا فَلَا يُسۡرِف فِّي ٱلۡقَتۡلِۖ إِنَّهُۥ كَانَ مَنصُورٗا

Wala msiuwe nafsi ambayo Allah amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 34

وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ بِٱلۡعَهۡدِۖ إِنَّ ٱلۡعَهۡدَ كَانَ مَسۡـُٔولٗا

Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi ni yenye kuulizwa



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 35

وَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ إِذَا كِلۡتُمۡ وَزِنُواْ بِٱلۡقِسۡطَاسِ ٱلۡمُسۡتَقِيمِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلٗا

Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na hatimaye ndio bora



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 36

وَلَا تَقۡفُ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۚ إِنَّ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡبَصَرَ وَٱلۡفُؤَادَ كُلُّ أُوْلَـٰٓئِكَ كَانَ عَنۡهُ مَسۡـُٔولٗا

Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa (vitaulizwa)



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 37

وَلَا تَمۡشِ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَرَحًاۖ إِنَّكَ لَن تَخۡرِقَ ٱلۡأَرۡضَ وَلَن تَبۡلُغَ ٱلۡجِبَالَ طُولٗا

Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima