Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 235

وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا عَرَّضۡتُم بِهِۦ مِنۡ خِطۡبَةِ ٱلنِّسَآءِ أَوۡ أَكۡنَنتُمۡ فِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمۡ سَتَذۡكُرُونَهُنَّ وَلَٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّآ أَن تَقُولُواْ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗاۚ وَلَا تَعۡزِمُواْ عُقۡدَةَ ٱلنِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡكِتَٰبُ أَجَلَهُۥۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Na si vibaya kwenu posa za fumbo mlizowafumbia au mlicho-kificha kwenye nafsi zenu. Allah amejua kuwa nyinyi mtawakumbuka hao, Na lakini msiwaahidi (ndoa) kwa siri isipokuwa mseme maneno mema. Na msiazimie kufunga nao ndoa mpaka Eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Allah anajua yaliyomo katika nafsi zenu, basi jihadharini naye, najueni kwamba Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 263

۞قَوۡلٞ مَّعۡرُوفٞ وَمَغۡفِرَةٌ خَيۡرٞ مِّن صَدَقَةٖ يَتۡبَعُهَآ أَذٗىۗ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَلِيمٞ

Kauli njema na kusamehe ni bora kuliko sadaka inayofuatishwa na maudhi, na Allah ni Mkwasi sana, Mpole mno



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 155

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ مِنكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ إِنَّمَا ٱسۡتَزَلَّهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ بِبَعۡضِ مَا كَسَبُواْۖ وَلَقَدۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Hakika Wale waliorudi miongoni mwenu siku ambayo majeshi mawili yalipokutana, hakika shetani (ndiye) aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyoyafanya, na kwa hakika Allah amewasamehe. Hakika Allah ni Msamehevu sana Mpole Mno



Sura: ANNISAI 

Aya : 12

۞وَلَكُمۡ نِصۡفُ مَا تَرَكَ أَزۡوَٰجُكُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٞ فَلَكُمُ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡنَۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِينَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۚ وَلَهُنَّ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡتُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّكُمۡ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَكُمۡ وَلَدٞ فَلَهُنَّ ٱلثُّمُنُ مِمَّا تَرَكۡتُمۚ مِّنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ تُوصُونَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۗ وَإِن كَانَ رَجُلٞ يُورَثُ كَلَٰلَةً أَوِ ٱمۡرَأَةٞ وَلَهُۥٓ أَخٌ أَوۡ أُخۡتٞ فَلِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُۚ فَإِن كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمۡ شُرَكَآءُ فِي ٱلثُّلُثِۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصَىٰ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍ غَيۡرَ مُضَآرّٖۚ وَصِيَّةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَلِيمٞ

Na nyinyi mna nusu ya kile walichoacha wake zenu kama hawakuwa na mtoto na kama wakiwa na mtoto, basi fungu lenu ni robo tu ya walichoacha baada ya kutekeleza wasia wanaoweka au deni. Na wake zenu wana robo ya mlicho kiacha ikiwa tu hamkuacha mtoto, na mkiwa na mtoto basi watapata thumni ya mlichokiacha baada ya kutekeleza wasia mnaoweka au deni. Na ikiwa mtu yeyote mwanaume au mwanamke atarithiwa na kaka yake au dada yake kwa kutoacha baba na mtoto, basi kila mmoja wao anafungu la sudusi, na kama watakuwa (ndugu) zaidi ya mmoja basi hao watashirikiana katika thuluthi[1] baada ya kutoa fungu la wasia uliowekwa au deni bila ya madhara. (hili) ni agizo kutoka kwa Allah na Allah ni Mjuzi sana Mpole mno


1- - Kaka na dada waliokusudiwa hapa ni wa upande wa mama kwa dalili kwamba kaka wa baba na mama au wa baba wanachukua kilichobaki baada ya watu wa mafungu na kama hakuna basi anachukua chote. Pia dada anarithi nusu ya mali hana fungu la theluthi, hivyo ni dhahiri hapa waliolengwa ni kaka au dada wa upande wa mama.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 101

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهَاۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Enyi mlioamini, msiulize mambo (ambayo) mkidhihirishiwa yanakuchukizeni. Na mkiyauliza wakati Qur’ani inateremshwa mtadhihirishiwa. (Msirudie) Allah ameshayasamehe hayo (mliyokwishauliza). Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno



Sura: YUNUS 

Aya : 11

۞وَلَوۡ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسۡتِعۡجَالَهُم بِٱلۡخَيۡرِ لَقُضِيَ إِلَيۡهِمۡ أَجَلُهُمۡۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Na lau kama Allah angewaha-rakishia watu shari kama wao wanavyoharakisha kheri, bila shaka muda wao (wa kuishi) ungekatishwa (wangekuwa wameangamizwa zamani). Basi tunawaacha wale wasioamini kukutana nasi (Siku ya Kiyama) wakitangatanga katika upotevu wao



Sura: ANNAHLI 

Aya : 61

وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلۡمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيۡهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Na lau Allah angewachukulia hatua watu kwasababu ya dhuluma yao, asingemuacha hata mnyama mmoja; Lakini anawasubirisha mpaka muda uliowekwa; Na utakapofika muda wao, hawataweza kuichelewesha saa moja na hawataweza kuiwahisha



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 44

تُسَبِّحُ لَهُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ ٱلسَّبۡعُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِيهِنَّۚ وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمۡدِهِۦ وَلَٰكِن لَّا تَفۡقَهُونَ تَسۡبِيحَهُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورٗا

Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye kusamehe



Sura: AL-KAHF 

Aya : 58

وَرَبُّكَ ٱلۡغَفُورُ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۖ لَوۡ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُواْ لَعَجَّلَ لَهُمُ ٱلۡعَذَابَۚ بَل لَّهُم مَّوۡعِدٞ لَّن يَجِدُواْ مِن دُونِهِۦ مَوۡئِلٗا

Na Mola wako Mlezi ni Msa-mehevu Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu waliyo yachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo



Sura: AL-HAJJ 

Aya : 59

لَيُدۡخِلَنَّهُم مُّدۡخَلٗا يَرۡضَوۡنَهُۥۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَلِيمٌ حَلِيمٞ

Bila ya shaka atawaingiza pahala watakapo paridhia. Na hakika Allah ni Mjuzi na Mpole



Sura: AL-AHZAAB 

Aya : 51

۞تُرۡجِي مَن تَشَآءُ مِنۡهُنَّ وَتُـٔۡوِيٓ إِلَيۡكَ مَن تَشَآءُۖ وَمَنِ ٱبۡتَغَيۡتَ مِمَّنۡ عَزَلۡتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكَۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن تَقَرَّ أَعۡيُنُهُنَّ وَلَا يَحۡزَنَّ وَيَرۡضَيۡنَ بِمَآ ءَاتَيۡتَهُنَّ كُلُّهُنَّۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَلِيمٗا

Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao, na umsogeze umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliye mtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unacho wapa wao wote. Na Allah anajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Allah ni Mwenye kujua, Mwenye hekima



Sura: FAATWIR 

Aya : 41

۞إِنَّ ٱللَّهَ يُمۡسِكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ أَن تَزُولَاۚ وَلَئِن زَالَتَآ إِنۡ أَمۡسَكَهُمَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنۢ بَعۡدِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورٗا

Hakika Allah ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe



Sura: FAATWIR 

Aya : 45

وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُواْ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهۡرِهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرَۢا

Na lau kuwa Allah angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Allah ni Mwenye kuwaona waja wake barabara



Sura: ATTAGHAABUN 

Aya : 17

إِن تُقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعِفۡهُ لَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ

Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni maradufu, na atakusameheni. Na Allah ni Mwenye kupokea shukurani, Mpole, (Mvumilivu)