Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 155

وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَيۡءٖ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٰتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Na kwa yakini kabisa, tutakutieni katika mtihani mdogo wa hofu na njaa na upungufu wa mali na uhai na matunda. Na wape bishara wenye uvumilivu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 156

ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٞ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ

Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika, sisi ni wa Allah, na kwake yeye tu tutarejea



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 214

أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَأۡتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُمۖ مَّسَّتۡهُمُ ٱلۡبَأۡسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلۡزِلُواْ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصۡرُ ٱللَّهِۗ أَلَآ إِنَّ نَصۡرَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ

Je, mmedhani kuwa mtaingia peponi ilhali haujakufikeni mfano wa ambao wamepita kabla yenu? Yaliwapata misukosuko na madhara na walitetemeshwa hadi akasema Mtume na walioamini pamoja naye kwamba: Ni lini itafika nusura ya Allah? Eleweni kwamba, hakika nusura ya Allah iko karibu mno



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 249

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Basi Twaluti alipoondoka na majeshi alisema: Hakika Allah atakufanyieni mtihani kwa mto, basi atakayekunywa humo si pamoja nami, na asiye yanywa bila shaka yupo pamoja nami, ila atakayeteka kiasi cha kiganja cha mkono wake. Basi walikunywa humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi alipovuka yeye na walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatumuwezi Jaluti na majeshi yake. Wakasema: wale ambao wana yakini ya kukutana na Allah: Makundi mangapi machache yameyashinda makundi mengi kwa idhini ya Allah? Na Allah yupo pamoja na wafanyao subira



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 152

وَلَقَدۡ صَدَقَكُمُ ٱللَّهُ وَعۡدَهُۥٓ إِذۡ تَحُسُّونَهُم بِإِذۡنِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَا فَشِلۡتُمۡ وَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَعَصَيۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَآ أَرَىٰكُم مَّا تُحِبُّونَۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلدُّنۡيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۚ ثُمَّ صَرَفَكُمۡ عَنۡهُمۡ لِيَبۡتَلِيَكُمۡۖ وَلَقَدۡ عَفَا عَنكُمۡۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na ni hakika kabisa, Allah alitimiza ahadi yake kwenu, pale mlivyokuwa mnawafyeka kwa idhini yake hadi mliposhindwa na mkazozana (nyinyi kwa nyinyi) kuhusu amri ya (Mtume) na mkaasi baada ya Allah kuwaonesheni kile mnachokipenda. Kati yenu wapo wanaotaka dunia, na wapo miongoni mwenu wanaotaka Akhera. Kisha akakugeuzeni toka kwao ili akujaribuni, na kwa hakika ameshakusameheni. Na Allah ni Mwenye fadhila kwa Waumini



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 179

مَّا كَانَ ٱللَّهُ لِيَذَرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَىٰ مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ ٱلۡخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُطۡلِعَكُمۡ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَجۡتَبِي مِن رُّسُلِهِۦ مَن يَشَآءُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ وَإِن تُؤۡمِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَلَكُمۡ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Haiwi kwa Allah awaache waumini katika hali mliyonayo mpaka awapambanue wabaya kutokana na wema, na haikuwa kwa Allah akujulisheni mambo yaliyofichikana, lakini Allah humteua katika Mitume wake amtakaye, basi muaminini Allah na Mitume wake, na mkiamini na mkamcha Allah, basi mtakuwa na ujira mkubwa mno



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 186

۞لَتُبۡلَوُنَّ فِيٓ أَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ وَلَتَسۡمَعُنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُوٓاْ أَذٗى كَثِيرٗاۚ وَإِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنۡ عَزۡمِ ٱلۡأُمُورِ

Na apa ya kuwa mtapewa mitihani katika mali zenu na nafsi zenu, na mtazisikia kero nyingi kutoka kwa waliopewa vitabu kabla yenu na kutoka kwa wale waliofanya ushirikina, na ikiwa mtavumilia na mkamcha Allah, basi hayo ndiyo mambo ya kuazimia



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 165

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَـٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمُۢ

Na yeye (Allah) ndiye aliyekufanyeni mnaopokezana duniani, na akawanyanyua baadhi yenu juu ya wengine kwa daraja ili akujaribuni katika yale aliyokupeni. Hakika, Mola wako Mlezi ni Mwepesi sana wa kuadhibu na, kwa hakika kabisa, yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Sura: AN-FAL 

Aya : 17

فَلَمۡ تَقۡتُلُوهُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمۡۚ وَمَا رَمَيۡتَ إِذۡ رَمَيۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ وَلِيُبۡلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡهُ بَلَآءً حَسَنًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Basi (Kwenye Siku ya Badri) hamkuwaua nyinyi (hao makafiri kwa nguvu na uhodari wenu) lakini Allah ndiye aliyewaua. Na wewe (Muhammad) hukutupa (na kuufikisha mchanga kwenye nyuso za makafiri), lakini Allah ndiye aliyetupa (aliyeufikisha mchanga na ukawapata makafiri), na ili awajaribu Waumini kutokana na hayo majaribio mazuri (kwa kuwapa neema ya ngawira walio hai na waliouawa wakiwa mashahidi). Hakika Allah ni Msikivu, Mjuzi sana



Sura: HUUD 

Aya : 7

وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَكَانَ عَرۡشُهُۥ عَلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۗ وَلَئِن قُلۡتَ إِنَّكُم مَّبۡعُوثُونَ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡمَوۡتِ لَيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na ni Yeye ambaye ameziumba mbingu na ardhi katika siku sita, na Arshi yake ilikuwa juu ya maji (kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi), ili awatahini (ajue) ni nani miongoni mwenu aliye mzuri sana wa matendo. Na endapo utawaambia: Hakika nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa, watasema wale waliokufuru: Hii Qur’ani sichochote ispokuwa ni uchawi tu ulio wazi



Sura: AL-ANKABUUT 

Aya : 2

أَحَسِبَ ٱلنَّاسُ أَن يُتۡرَكُوٓاْ أَن يَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا وَهُمۡ لَا يُفۡتَنُونَ

Je, watu walidhani wataachwa waseme: Tumeamini na wasija-ribiwe?



Sura: AL-ANKABUUT 

Aya : 3

وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Na kwa hakika kabisa, tuliwajaribu waliokuwepo kabla yao, basi kwa yakini kabisa Allah atawatambua ambao wamesema kweli na atawatambua waongo



Sura: AL-AHZAAB 

Aya : 11

هُنَالِكَ ٱبۡتُلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَزُلۡزِلُواْ زِلۡزَالٗا شَدِيدٗا

Hapo ndipo Waumini walipo jaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali



Sura: MUHAMMAD 

Aya : 31

وَلَنَبۡلُوَنَّكُمۡ حَتَّىٰ نَعۡلَمَ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ مِنكُمۡ وَٱلصَّـٰبِرِينَ وَنَبۡلُوَاْ أَخۡبَارَكُمۡ

Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapiganao Jihadi katika nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu



Sura: ATTAGHAABUN 

Aya : 15

إِنَّمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَأَوۡلَٰدُكُمۡ فِتۡنَةٞۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Hakika Mali zenu na watoto wenu ni jaribio. Na Kwa Allah upo ujira mkubwa



Sura: AL-MULK 

Aya : 2

ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ

Ambaye ameumba kifo na uhai ili akujaribuni; Ni nani miongoni mwenu mwenye kutenda (vitendo) vizuri zaidi? Na yeye (Allah) ndiye hasa Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kusamehe sana