Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 25

وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡهَا مِن ثَمَرَةٖ رِّزۡقٗا قَالُواْ هَٰذَا ٱلَّذِي رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَٰبِهٗاۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَهُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na wape bishara wale walioamini na kufanya matendo mema kuwa, watapata bustani zitiririkazo mito chini yake. Kila wanapopewa riziki ya matunda humo wanasema: Hii ndio ile riziki tuliyopewa kabla. Na wamepewa riziki hiyo ikiwa inafanana. Na watapata humo wake waliotwaharishwa, na watabaki humo daima



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 134

تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Huo ni umma umeshapita. Utapata ulicho kichuma na nyinyi mtapata mlicho kichuma. Na hamtaulizwa kuhusu waliyokuwa wakiyafanya



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 141

تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Huo ni umma umeshapita. Utapata ulichokichuma na nyinyi mtapata mlichokichuma. Na hamtaulizwa kuhusu waliyokuwa wakiyafanya



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 167

وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُواْ لَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةٗ فَنَتَبَرَّأَ مِنۡهُمۡ كَمَا تَبَرَّءُواْ مِنَّاۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ ٱللَّهُ أَعۡمَٰلَهُمۡ حَسَرَٰتٍ عَلَيۡهِمۡۖ وَمَا هُم بِخَٰرِجِينَ مِنَ ٱلنَّارِ

Na watasema wale waliofuata: Laiti tungeweza kurudi (duniani) tukawakataa kama wanavyotukataa. Hivi ndivyo Allah atakavyowaonesha vitendo vyao kuwa majuto kwao, na hawatakuwa wenye kutoka motoni



Sura: ANNISAI 

Aya : 123

لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Sio kwa matamanio yenu wala matamanio ya Watu wa Kitabu. Yeyote anayefanya uovu atalipwa kwa uovu huo, na wala hatapata yeyote wa kumlinda na wa kumnusuru badala ya Allah



Sura: ANNISAI 

Aya : 124

وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَـٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا

Na yeyote anayefanya mema awe mwanaume au mwanamke na ilhali ni Muumini, basi hao wataingia Peponi na hawatadhulumiwa (jema lolote) hata kama liwe ujazo wa uwazi wa tundu ya kokwa ya tende



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 9

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٌ عَظِيمٞ

Allah amewaahidi walioamini na kutenda mema (kwamba) watapata msamaha na malipo makubwa sana



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 33

إِنَّمَا جَزَـٰٓؤُاْ ٱلَّذِينَ يُحَارِبُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوٓاْ أَوۡ يُصَلَّبُوٓاْ أَوۡ تُقَطَّعَ أَيۡدِيهِمۡ وَأَرۡجُلُهُم مِّنۡ خِلَٰفٍ أَوۡ يُنفَوۡاْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِۚ ذَٰلِكَ لَهُمۡ خِزۡيٞ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Kwa hakika kabisa, malipo ya wale wanaopigana vita na Allah na Mtume wake[1] na wanakwenda kasi katika kufanya uharibifu duniani ni kuuawa bila ya huruma au kusulubiwa au kukatwa katwa mikono yao na miguu yao kwa kupishana au kutolewa katika nchi (na kupelekwa uhamishoni). Hiyo ni kwa sababu wanastahiki hizaya (fedheha) duniani, na huko Akhera watapata adhabu kubwa mno


1- - Kinachokusudiwa hapa ni kuupiga vita Uislamu na Waislamu.


Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 132

وَلِكُلّٖ دَرَجَٰتٞ مِّمَّا عَمِلُواْۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ

Na wote miongoni mwao (majini na binadamu) wana madaraja kutokana na waliyoyatenda, na Mola wako si Mwenye kughafilika na yote wanayotenda



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 160

مَن جَآءَ بِٱلۡحَسَنَةِ فَلَهُۥ عَشۡرُ أَمۡثَالِهَاۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَا وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Yeyote atendae (jambo) zuri atapata mfano wa zuri hilo mara kumi, na atendae baya hatalipwa isipokuwa mfano wake, na wao (waja) hawatadhulumiwa



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 43

وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلّٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَقَالُواْ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي هَدَىٰنَا لِهَٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهۡتَدِيَ لَوۡلَآ أَنۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُۖ لَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّۖ وَنُودُوٓاْ أَن تِلۡكُمُ ٱلۡجَنَّةُ أُورِثۡتُمُوهَا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na tutaondoa husuda vifuani mwao, ikipita mito chini yao na watasema: “Kila sifa njema anaistahiki Allah ambaye ametuongoza kwenye hili na tusingeweza kuongoka kama Allah asingetuongoza”. Hakika kabisa, Mitume ya Allah imekuja kwa haki. Na (waumini huko peponi) wataitwa (na kuambiwa kwamba): Hii ndio pepo mliorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya



Sura: HUUD 

Aya : 15

مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيۡهِمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ فِيهَا وَهُمۡ فِيهَا لَا يُبۡخَسُونَ

Wale wanaotaka (katika matendo yao wanayofanya wapate) maisha ya kidunia na mapambo yake (kama dhahabu, fedha, watoto nafasi, wanawake nk), tutawalipa (thawabu hizo) kikamilifu hapa duniani na hawatapunguziwa chochote



Sura: HUUD 

Aya : 16

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَيۡسَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا ٱلنَّارُۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hao ndio wale ambao Akhera hawana chochote isipokuwa Moto tu, na yataharibika matendo yao yote na ni batili yote waliyokuwa wakiyatenda



Sura: HUUD 

Aya : 111

وَإِنَّ كُلّٗا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمۡ رَبُّكَ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na hakika kila kaumu (zilizotajwa) watalipwa malipo yao kamili. Hakika Yeye kwa yote myatendayo anayo habari



Sura: ANNAHLI 

Aya : 93

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na Allah angelitaka, kwa yakini angeliwafanyeni umma moja; lakini anayetaka (upotevu) anampoteza, na anayetaka (mwongozo) anamwongoza; na hakika mtaulizwa yale mliyokuwa mkiyafanya



Sura: ANNAHLI 

Aya : 97

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Atakayefanya mema, mwana-mume au mwanamke, ilhali ni muumini, basi kwa hakika tutampa maisha mema na kwa yakini tutawapa ujira wao kwa uzuri zaidi kuliko yale waliokuwa wakiyatenda



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 19

وَمَنۡ أَرَادَ ٱلۡأٓخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعۡيَهَا وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَـٰٓئِكَ كَانَ سَعۡيُهُم مَّشۡكُورٗا

Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a’mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa



Sura: AL-KAHF 

Aya : 30

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ مَنۡ أَحۡسَنَ عَمَلًا

Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema



Sura: AL-KAHF 

Aya : 31

أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ جَنَّـٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيهَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٖ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرٗا مِّن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقٗا

Hao watapata Bustani za milele, zinazo pita mito kati yake. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na at’ilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi. Ni malipo bora hayo! Na matandiko mazuri mno ya kupumzikia!



Sura: AL-KAHF 

Aya : 49

وَوُضِعَ ٱلۡكِتَٰبُ فَتَرَى ٱلۡمُجۡرِمِينَ مُشۡفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَٰوَيۡلَتَنَا مَالِ هَٰذَا ٱلۡكِتَٰبِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةٗ وَلَا كَبِيرَةً إِلَّآ أَحۡصَىٰهَاۚ وَوَجَدُواْ مَا عَمِلُواْ حَاضِرٗاۗ وَلَا يَظۡلِمُ رَبُّكَ أَحَدٗا

Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila isipokuwa limelisajiliwa? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote



Sura: AL-KAHF 

Aya : 103

قُلۡ هَلۡ نُنَبِّئُكُم بِٱلۡأَخۡسَرِينَ أَعۡمَٰلًا

Sema: Je, tukutajieni wenye hasara mno katika vitendo vyao?



Sura: AL-KAHF 

Aya : 104

ٱلَّذِينَ ضَلَّ سَعۡيُهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُمۡ يَحۡسَبُونَ أَنَّهُمۡ يُحۡسِنُونَ صُنۡعًا

Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri



Sura: AL-KAHF 

Aya : 105

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ وَلِقَآئِهِۦ فَحَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَلَا نُقِيمُ لَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَزۡنٗا

Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawathamini kitu



Sura: AL-KAHF 

Aya : 106

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُمۡ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُواْ وَٱتَّخَذُوٓاْ ءَايَٰتِي وَرُسُلِي هُزُوًا

Hiyo Jahannamu ni malipo yao kwa walivyo kufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu



Sura: AL-KAHF 

Aya : 107

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ كَانَتۡ لَهُمۡ جَنَّـٰتُ ٱلۡفِرۡدَوۡسِ نُزُلًا

Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi



Sura: AL-KAHF 

Aya : 108

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يَبۡغُونَ عَنۡهَا حِوَلٗا

Watadumu humo; hawatataka kuondoka



Sura: TWAHA 

Aya : 15

إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ

Hakika Saa (Kiyama) kitakuja bila ya shaka. Nimekaribia kukificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyo yafanya



Sura: TWAHA 

Aya : 74

إِنَّهُۥ مَن يَأۡتِ رَبَّهُۥ مُجۡرِمٗا فَإِنَّ لَهُۥ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ

Hakika atakayemjia Mola wake Mlezi naye ni muovu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi



Sura: TWAHA 

Aya : 75

وَمَن يَأۡتِهِۦ مُؤۡمِنٗا قَدۡ عَمِلَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَأُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلدَّرَجَٰتُ ٱلۡعُلَىٰ

Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu



Sura: AL-ANBIYAA 

Aya : 94

فَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَا كُفۡرَانَ لِسَعۡيِهِۦ وَإِنَّا لَهُۥ كَٰتِبُونَ

Na atendaye mema naye ni Muumini basi haitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisi tunamwandikia