Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 102

وَٱتَّبَعُواْ مَا تَتۡلُواْ ٱلشَّيَٰطِينُ عَلَىٰ مُلۡكِ سُلَيۡمَٰنَۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيۡمَٰنُ وَلَٰكِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ كَفَرُواْ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحۡرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلۡمَلَكَيۡنِ بِبَابِلَ هَٰرُوتَ وَمَٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنۡ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحۡنُ فِتۡنَةٞ فَلَا تَكۡفُرۡۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنۡهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيۡنَ ٱلۡمَرۡءِ وَزَوۡجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنۡ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡۚ وَلَقَدۡ عَلِمُواْ لَمَنِ ٱشۡتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖۚ وَلَبِئۡسَ مَا شَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na wamefuata yale yanayoso-mwa na Mashetani katika (wakati wa) ufalme wa Suleimani. Na Suleimani hakukufuru, lakini Mashetani ndio waliokufuru; (kwa sababu) wanawafundisha watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili Haruta na Maruta katika mji wa Babil. Na wala hawamfundishi yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru. Basi wakajifunza kwao yale yawezayo kumfarakanisha mtu na mkewe. Na wala wao hawana uwezo wa kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Allah tu. Na wanajifunza yale yanayowadhuru na wala hayawanufaishi. Na kwa yakini wamejua kwamba aliyechagua haya hatakuwa na fungu lolote Akhera. Na nikibaya mnokilewalichozichagulianafsizao laiti wangekuwa wanajua



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 71

قُلۡ أَنَدۡعُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعۡقَابِنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِي ٱسۡتَهۡوَتۡهُ ٱلشَّيَٰطِينُ فِي ٱلۡأَرۡضِ حَيۡرَانَ لَهُۥٓ أَصۡحَٰبٞ يَدۡعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلۡهُدَى ٱئۡتِنَاۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۖ وَأُمِرۡنَا لِنُسۡلِمَ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Sema: Hivi tuwaombe (tuwaa-budu) badala ya Allah (Miungu) ambao hawatunufaishi na hawatudhuru na turudishwe nyuma (kwenye itikadi potofu tulizokwisha ziacha) baada ya Allah kutuongoa kama yule ambaye mashetani wamempagawisha katika ardhi, akiduwaa, akiwa na marafiki wanaomuita aende katika uongofu (wakimwambia): Njoo kwetu?[1] Sema: Hakika, muongozo wa Allah ndio uongofu, na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote


1- - Aya hapa inamtaka Muumini kuwa na msimamo imara na thabiti katika Imani na itikadi yake. Hatakiwi kuyumba au kuyumbishwa. Sio kila analolisikia au kuliona au kushawishiwa alifuate.


Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 112

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا شَيَٰطِينَ ٱلۡإِنسِ وَٱلۡجِنِّ يُوحِي بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ زُخۡرُفَ ٱلۡقَوۡلِ غُرُورٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ

Na kama hivyo tumemuwekea kila Nabii adui; mashetani watu na (mashetani) majini, wao kwa wao wakipeana maneno ya kupamba pamba kwa kudanganyana. Na lau kama Mola wako angetaka, wasingeyafanya hayo. Basi waache na hayo wayazushayo



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 121

وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ

Na msile (nyama ya mnyama) ambaye halikutajwa jina la Allah juu yake (wakati wa kuchinjwa), na hakika hilo (la kula nyama ya mnyama ambaye hakuchinjwa kwa taratibu za Kiislamu) ni uasi. Na hakika, mashetani wanatia ushawishi kwa marafiki zao (wa kibinadamu) ili wajadiliane nanyi (katika ulaji wa nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu). Na kama mkiwatii (katika kuhalalisha nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu) kwa hakika kabisa nyinyi ni washirikina (makafiri)



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 27

يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٰتِهِمَآۚ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ

Enyi Wanadamu, kamwe shetani asikufitinisheni[1] kama alivyowatoa Peponi wazazi wenu, akiwavua nguo zao ili kuwawekea wazi tupu zao. Hakika yeye (shetani) anakuoneni yeye na jeshi lake katika namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika, sisi tumewafanya mashetani wandani wa (watu) wasioamini


1- - Shetani asikudanganyeni kwa kukupambieni maasi, kama ambavyo alimhadaa baba yenu Adamu na mkewe kwa kuwashawishi waonje mti. Matokeo yake walitolewa Peponi.


Sura: AL-AARAAF 

Aya : 30

فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلضَّلَٰلَةُۚ إِنَّهُمُ ٱتَّخَذُواْ ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُم مُّهۡتَدُونَ

Kundi moja (Allah) ameliongoa na kundi (lingine) limestahiki kupotea. Hakika, wao wamewafanya mashetani wandani (wao) badala ya Allah na wanadhani kwamba wameongoka



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 27

إِنَّ ٱلۡمُبَذِّرِينَ كَانُوٓاْ إِخۡوَٰنَ ٱلشَّيَٰطِينِۖ وَكَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لِرَبِّهِۦ كَفُورٗا

Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashetani. Na Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi



Sura: MARYAM 

Aya : 68

فَوَرَبِّكَ لَنَحۡشُرَنَّهُمۡ وَٱلشَّيَٰطِينَ ثُمَّ لَنُحۡضِرَنَّهُمۡ حَوۡلَ جَهَنَّمَ جِثِيّٗا

Basi naapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashetani; kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu, nao wamepiga magoti



Sura: MARYAM 

Aya : 83

أَلَمۡ تَرَ أَنَّآ أَرۡسَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ تَؤُزُّهُمۡ أَزّٗا

Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashetani kwa makafiri wawachochee kwa uchochezi?



Sura: AL-ANBIYAA 

Aya : 82

وَمِنَ ٱلشَّيَٰطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُۥ وَيَعۡمَلُونَ عَمَلٗا دُونَ ذَٰلِكَۖ وَكُنَّا لَهُمۡ حَٰفِظِينَ

Na pia mashetani wanao mpigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo. Na Sisi tulikuwa walinzi wao



Sura: AL-HAJJ 

Aya : 3

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيۡطَٰنٖ مَّرِيدٖ

Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Allah bila ya elimu, na wanamfuata kila shetani aliyeasi



Sura: AL-HAJJ 

Aya : 4

كُتِبَ عَلَيۡهِ أَنَّهُۥ مَن تَوَلَّاهُ فَأَنَّهُۥ يُضِلُّهُۥ وَيَهۡدِيهِ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ

Ameandikiwa kwamba anaye mfanya kuwa rafiki, basi huyo hakika atampoteza na atamwongoza kwenye adhabu ya Moto mkali



Sura: ALMUUMINUUN 

Aya : 97

وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنۡ هَمَزَٰتِ ٱلشَّيَٰطِينِ

Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashetani



Sura: ALMUUMINUUN 

Aya : 98

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحۡضُرُونِ

Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 210

وَمَا تَنَزَّلَتۡ بِهِ ٱلشَّيَٰطِينُ

Wala Mashet’ani hawakuteremka nayo,



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 221

هَلۡ أُنَبِّئُكُمۡ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَٰطِينُ

Je! Nikwambieni nani wana-washukia Mashet’ani?



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 222

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٖ

Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 223

يُلۡقُونَ ٱلسَّمۡعَ وَأَكۡثَرُهُمۡ كَٰذِبُونَ

Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 7

وَحِفۡظٗا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ مَّارِدٖ

Na kwa ajili ya ulinzi dhidi ya kila shetani muasi



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 8

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٖ

Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 9

دُحُورٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ وَاصِبٌ

Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 10

إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ ثَاقِبٞ

Isipo kuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfuatia kimondo kinacho ng’ara



Sura: SWAAD 

Aya : 37

وَٱلشَّيَٰطِينَ كُلَّ بَنَّآءٖ وَغَوَّاصٖ

Na tukayafanya mashetani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi



Sura: SWAAD 

Aya : 38

وَءَاخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي ٱلۡأَصۡفَادِ

Na wengine wafungwao kwa minyororo



Sura: AL-MULK 

Aya : 5

وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَٰبِيحَ وَجَعَلۡنَٰهَا رُجُومٗا لِّلشَّيَٰطِينِۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ

Na kwa hakika, tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa (nyota), na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia (hao mashetani) adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu