Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 236

لَّا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِن طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ مَا لَمۡ تَمَسُّوهُنَّ أَوۡ تَفۡرِضُواْ لَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى ٱلۡمُوسِعِ قَدَرُهُۥ وَعَلَى ٱلۡمُقۡتِرِ قَدَرُهُۥ مَتَٰعَۢا بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Hakuna ubaya kwenu endapo mtawaacha wake kabla ya kuwaingilia na kuwakadiria mahari yao. Na wapeni cha kuwaliwaza (kitoka nyumba). Mwenye uwezo mkubwa atoe kulingana na uwezo wake, na mwenye uwezo mdogo atoe kulingana na uwezo alionao. Niliwazo litolewalo kwa wema na ni haki kwa watendao mazuri



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 237

وَإِن طَلَّقۡتُمُوهُنَّ مِن قَبۡلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدۡ فَرَضۡتُمۡ لَهُنَّ فَرِيضَةٗ فَنِصۡفُ مَا فَرَضۡتُمۡ إِلَّآ أَن يَعۡفُونَ أَوۡ يَعۡفُوَاْ ٱلَّذِي بِيَدِهِۦ عُقۡدَةُ ٱلنِّكَاحِۚ وَأَن تَعۡفُوٓاْ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۚ وَلَا تَنسَوُاْ ٱلۡفَضۡلَ بَيۡنَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Na endapo mtawaacha kabla ya kuwaingilia na ilhali mmekwisha kadiria mahari, basi wapeni nusu ya mahari mliokadiria, isipokuwa kama wake wenyewe watasamehe au atasamehe yule ambaye kifungo cha ndoa kipo mikononi mwake. Na kama mtasamehe, hilo liko karibu zaidi na Ucha Mungu. Na msisahau utu kati yenu. Hakika, Allah ni Mwenye kuyaona myatendayo



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 241

وَلِلۡمُطَلَّقَٰتِ مَتَٰعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ

Na wapeni wanawake wali-oachwa kiliwazo (kitoka nyumba) kwa wema, ikiwa ni haki kwa wam-chao Allah



Sura: ANNISAI 

Aya : 20

وَإِنۡ أَرَدتُّمُ ٱسۡتِبۡدَالَ زَوۡجٖ مَّكَانَ زَوۡجٖ وَءَاتَيۡتُمۡ إِحۡدَىٰهُنَّ قِنطَارٗا فَلَا تَأۡخُذُواْ مِنۡهُ شَيۡـًٔاۚ أَتَأۡخُذُونَهُۥ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا

Na endapo mtataka kubadili mke sehemu ya mke aliyepo na mmoja wao mkampa mali nyingi basi msichukuwe katika mali hiyo chochote. mnakichukuaje kwa uongo na dhambi za wazi



Sura: ANNISAI 

Aya : 21

وَكَيۡفَ تَأۡخُذُونَهُۥ وَقَدۡ أَفۡضَىٰ بَعۡضُكُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ وَأَخَذۡنَ مِنكُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا

Na mnazichukuaje ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na (wake) wamechukuwa kwenu ahadi nzito (ya kuishi kwa wema)



Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحۡصُواْ ٱلۡعِدَّةَۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ رَبَّكُمۡۖ لَا تُخۡرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخۡرُجۡنَ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ لَا تَدۡرِي لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحۡدِثُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ أَمۡرٗا

Ee Nabii, mnapotaka kuwapa talaka wanawake (wake zenu), basi wapeni talaka (katika wakati wa Twahara) kwenda kwenye Eda zao.[1]. Na hesabuni barabara eda na mcheni Allah Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio wazi. Na hiyo ndio mipaka ya Allah. Na yeyote atakayevuka mipaka ya Allah basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huwenda Allah akaibua (akaleta) jambo (jingine) baada ya hayo


1- - (Yaani wakati wakiwa twahara kabla ya kuwaingilia)


Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 2

فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ فَارِقُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖ وَأَشۡهِدُواْ ذَوَيۡ عَدۡلٖ مِّنكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَ لِلَّهِۚ ذَٰلِكُمۡ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مَخۡرَجٗا

Na watakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allah. Hivyo ndivyo anavyo waidhiwa (anavyo agizwa) anaye mwamini Allah na Siku ya Mwisho. Na yeyote anayemcha Allah; humtengenezea njia ya kutokea (kwenye shida)



Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 3

وَيَرۡزُقۡهُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَحۡتَسِبُۚ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَٰلِغُ أَمۡرِهِۦۚ قَدۡ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَيۡءٖ قَدۡرٗا

Na humruzuku kwa njia asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Allah Yeye humtosha. Hakika Allah anatimiza amri yake. Hakika Allah Amejaalia kwa kila kitu na makadirio yake



Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 4

وَٱلَّـٰٓـِٔي يَئِسۡنَ مِنَ ٱلۡمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمۡ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَٰثَةُ أَشۡهُرٖ وَٱلَّـٰٓـِٔي لَمۡ يَحِضۡنَۚ وَأُوْلَٰتُ ٱلۡأَحۡمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مِنۡ أَمۡرِهِۦ يُسۡرٗا

Na wale wanawake ambao wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao. Na yeyote anayemcha Allah Atamjaalia wepesi katika jambo lake



Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 5

ذَٰلِكَ أَمۡرُ ٱللَّهِ أَنزَلَهُۥٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُعۡظِمۡ لَهُۥٓ أَجۡرًا

Hiyo ni amri ya Allah Amekuteremshieni; na yeyote anayemcha Allah, Atamfutia maovu yake, na atampa ujira ulio mkubwa



Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 6

أَسۡكِنُوهُنَّ مِنۡ حَيۡثُ سَكَنتُم مِّن وُجۡدِكُمۡ وَلَا تُضَآرُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُواْ عَلَيۡهِنَّۚ وَإِن كُنَّ أُوْلَٰتِ حَمۡلٖ فَأَنفِقُواْ عَلَيۡهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ فَإِنۡ أَرۡضَعۡنَ لَكُمۡ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَأۡتَمِرُواْ بَيۡنَكُم بِمَعۡرُوفٖۖ وَإِن تَعَاسَرۡتُمۡ فَسَتُرۡضِعُ لَهُۥٓ أُخۡرَىٰ

Wawekeni wanawake (mlio-wataliki) kwenye majumba mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu, na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wapeni matumizi mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni (Watoto wenu), basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni baina yenu kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine



Sura: ATTWALAAQ 

Aya : 7

لِيُنفِقۡ ذُو سَعَةٖ مِّن سَعَتِهِۦۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيۡهِ رِزۡقُهُۥ فَلۡيُنفِقۡ مِمَّآ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا مَآ ءَاتَىٰهَاۚ سَيَجۡعَلُ ٱللَّهُ بَعۡدَ عُسۡرٖ يُسۡرٗا

Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allah. Allah Hamkalifishi mtu yeyote yule isipokuwa kwa kile Alichompa. Allah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi