Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 42

وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na msichanganye haki na batili na msifiche haki na ilhali mnajua



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 92

۞وَلَقَدۡ جَآءَكُم مُّوسَىٰ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ

Na kwa hakika kabisa, alikujieni Musa akiwa na miujiza ya wazi, kisha baada yake[1] mkamfanya Ndama (Mungu) na ilhali nyinyi ni wenye kudhulumu (nafsi zenu)


1- - Baada ya Musa kwenda kwenye kiaga cha kukutana na Mola wake


Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 93

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱسۡمَعُواْۖ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَأُشۡرِبُواْ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡعِجۡلَ بِكُفۡرِهِمۡۚ قُلۡ بِئۡسَمَا يَأۡمُرُكُم بِهِۦٓ إِيمَٰنُكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi yenu na tukauinua (mlima) Turi juu yenu (tukakuambieni): Yashikeni kwa nguvu tuliyokupeni na sikilizeni. Wakasema: Tumesikia na tumeasi, na wakanyweshwa mioyoni mwao (kupenda) kuabudu ndama kwa sababu ya kufuru zao. Waambie: Ni jambo baya sana inavyokuamrisheni imani yenu, kama ninyi ni waumini



Sura: ANNISAI 

Aya : 50

ٱنظُرۡ كَيۡفَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثۡمٗا مُّبِينًا

Tazama jinsi wanavyomtungia Allah uongo. Na hayo yanatosha kuwa dhambi zilizo dhahiri



Sura: ANNISAI 

Aya : 117

إِن يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ إِنَٰثٗا وَإِن يَدۡعُونَ إِلَّا شَيۡطَٰنٗا مَّرِيدٗا

Hawaombi (hawaabudu) badala yake isipokuwa tu wanawake (masanamu)[1], na hawamuombi isipokuwa shetani (Ibilisi) aliyechupa mipaka (katika uasi)


1- - Masanamu hapa yameitwa wanawake sio kwa lengo la kudhalilisha wanawake lakini ni kunukuu hali halisi ya masanamu hayo kwa mujibu wa makafiri wenyewe waliyoyatengeneza. Wanachuoni wametoa ufafanuzi kwamba, masanamu hapa yameitwa wanawake kwa tafsiri mbili.
1. Tafsiri ya kwanza ni kwamba makafiri waliyapa masanamu yao majina ya kike, kama vile Lata, Uza, Manata n.k.
2. Tafsiri ya pili ni kwamba masanamu yameitwa wanawake kwa sababu ya udhaifu wake wa kutoweza kujihami kama ilivyo kwa wanawake.


Sura: ANNISAI 

Aya : 118

لَّعَنَهُ ٱللَّهُۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنۡ عِبَادِكَ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا

Allah amemlaani (shetani). Na amesema (baada ya kulaaniwa): Kwa yakini kabisa, nitachukua katika waja wako fungu lililokadiriwa



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 103

مَا جَعَلَ ٱللَّهُ مِنۢ بَحِيرَةٖ وَلَا سَآئِبَةٖ وَلَا وَصِيلَةٖ وَلَا حَامٖ وَلَٰكِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَأَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Allah hakuweka uharamu (wowote) katika Bahira[1] wala Saiba[2] wala Waswila[3] wala Hami.[4] Na lakini wale waliokufuru wanamzushia Allah uwongo, na wengi wao hawatumii akili


1- - Bahira ni jina la ngamia jike aliyetogwa masikio na kuachwa huru aende malishoni bila ya mchungaji.
Wapagani wa Kikuraishi na hasa kabila la Khuzaa walimtukuza Ngamia huyu na kumfanya maalumu kwa
ajili ya ibada za masanamu; habebeshwi kitu mgongoni kwake, ngozi yake haitiwi alama na maziwa
yake hunywewa na mgeni tu.

2- - Saiba ni ngamia aliyewekwa nadhiri kwa ajili ya masanamu pindi mtu anaposalimika na maradhi
au kupata hadhi fulani. Ngamia huyu pia aliachwa huru aende malishoni bila ya mchungaji na ilikuwa
marufuku kupandwa na yeyote, isipokuwa haikatazwi kumtumia katika kubeba majani ya malisho na utekaji maji.

3- - Waswila katika ngamia ni ngamia jike aliyeachwa huru. Na Waswila katika mbuzi au kondoo ni yule
aliyezaa majike kwa mfululizo.

4- - Hami ni fahali (dume) la ngamia lililozalisha zao nyingi na kuzeeka. Halipandwi kama chombo cha usafiri wala halibebeshwi mizigo na huachwa huru kwenda machungani bila ya mchungaji.


Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 21

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia uongo Allah au aliyezipinga Aya zake? Hakika ni kuwa, madhalimu hawafaulu



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 74

۞وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ ءَازَرَ أَتَتَّخِذُ أَصۡنَامًا ءَالِهَةً إِنِّيٓ أَرَىٰكَ وَقَوۡمَكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Na (kumbuka Mtume) Ibrahimu alipomwambia baba yake Azar (kwamba): Hivi unayafanya masanamu Miungu? Hakika, mimi ninakuona wewe na watu wako kwamba mmo katika upotevu ulio wazi



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 93

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمۡ يُوحَ إِلَيۡهِ شَيۡءٞ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثۡلَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّـٰلِمُونَ فِي غَمَرَٰتِ ٱلۡمَوۡتِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ بَاسِطُوٓاْ أَيۡدِيهِمۡ أَخۡرِجُوٓاْ أَنفُسَكُمُۖ ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَوۡنَ عَذَابَ ٱلۡهُونِ بِمَا كُنتُمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَكُنتُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِهِۦ تَسۡتَكۡبِرُونَ

Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzushia Allah uongo (kuwa amempa Utume) au aliyesema kuwa: Nimeletewa Wahyi na ilhali hakuletewa Wahyi wowote? Na (ni nani dhalimu zaidi kuliko) yule aliyesema kuwa: Nitateremsha mfano wa aliyoteremsha Allah? Na lau ungeona wakati madhalimu wamo katika mahangaiko ya mauti na Malaika wamenyoosha mikono yao (wakiwa tayari kuchukua roho zao wakiwaambia): Zitoeni (ziokoeni) roho zenu (kutoka mikononi mwetu kama mnaweza kwa sababu) leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya yale yasiyokuwa ya haki mliyomsingizia Allah, na mlikuwa mnazifanyia kiburi Aya zake



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 94

وَلَقَدۡ جِئۡتُمُونَا فُرَٰدَىٰ كَمَا خَلَقۡنَٰكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَتَرَكۡتُم مَّا خَوَّلۡنَٰكُمۡ وَرَآءَ ظُهُورِكُمۡۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمۡ شُفَعَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُمۡ أَنَّهُمۡ فِيكُمۡ شُرَكَـٰٓؤُاْۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيۡنَكُمۡ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ

Na kwa hakika kabisa, mmetujia (mkiwa) wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza, na mmeyaacha nyuma yenu yote tuliyokupeni, na hatuoni mkiwa pamoja nao (wale) waombezi wenu ambao mlidai kuwa mna ushirika nao. Kwa hakika kabisa, mafungamano kati yenu yamekatika, na yamekupoteeni mliyokuwa mnadai



Sura: AL-AN’AAM 

Aya : 108

وَلَا تَسُبُّواْ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَسُبُّواْ ٱللَّهَ عَدۡوَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرۡجِعُهُمۡ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na msiwatukane wale wanao omba (wanaoabudu vitu vingine) badala ya Allah, ikawa sababu ya wao kumtukana Allah bila ya elimu yoyote (kwa ufedhuli)[1]. Kama hivyo tumefanyia kila watu waone mazuri matendo yao. Kisha ni kwa Mola wao tu marejeo yao na atawaambia yote waliyokuwa wakiyatenda


1- - Hapa Waislamu wanakatazwa kutukana wafuasi wa dini nyingine, jambo linaloweza kusababisha wanaotukanwa kujibu mapigo na hatimae nao kumtukana Allah au Mtume na kupelekea kuvunjika kwa amani na utulivu. Ama kuhubiri kwa hekima na mawaidha mazuri, kujadiliana kwa namna nzuri ni jambo linalotakiwa kufanywa.


Sura: AL-AARAAF 

Aya : 138

وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتَوۡاْ عَلَىٰ قَوۡمٖ يَعۡكُفُونَ عَلَىٰٓ أَصۡنَامٖ لَّهُمۡۚ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱجۡعَل لَّنَآ إِلَٰهٗا كَمَا لَهُمۡ ءَالِهَةٞۚ قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ

Na tuliwavusha Wana wa Israili baharini, wakafika kwa watu wanaoabudu masanamu yao. (Wana wa Israili) Wakasema (kumwambia Mtume Musa): Ewe Musa, na sisi tufanyie Mungu kama hawa walivyo na Miungu. (Musa) Akasema: Hakika, nyinyi ni watu wajinga!



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 139

إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ مُتَبَّرٞ مَّا هُمۡ فِيهِ وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hakika, hawa kimeangamizwa ambacho wanakifanya na ni batili yote ambayo waliyokuwa wakiyatenda



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 148

وَٱتَّخَذَ قَوۡمُ مُوسَىٰ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِنۡ حُلِيِّهِمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٌۚ أَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّهُۥ لَا يُكَلِّمُهُمۡ وَلَا يَهۡدِيهِمۡ سَبِيلًاۘ ٱتَّخَذُوهُ وَكَانُواْ ظَٰلِمِينَ

Na watu Musa baada ya kuondoka kwake, walitengeneza kutokana na mapambo yao umbo la ndama lenye sauti (ya mlio wa ng’ombe). Hivi hawakuona kuwa (ndama yule) hawasemeshi na hawaongozi njia yoyote? Walimchukua (walimfanya kama Mungu) na walikuwa madhalimu



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 149

وَلَمَّا سُقِطَ فِيٓ أَيۡدِيهِمۡ وَرَأَوۡاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ ضَلُّواْ قَالُواْ لَئِن لَّمۡ يَرۡحَمۡنَا رَبُّنَا وَيَغۡفِرۡ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na walipoangukia mikononi mwao (walipojuta) na kuona kuwa wameshapotea walisema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hatatuhurumia na kutusamehe, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kupata hasara



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 152

إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ ٱلۡعِجۡلَ سَيَنَالُهُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَذِلَّةٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُفۡتَرِينَ

Hakika, wale waliomfanya ndama (Mungu) itawapata adhabu ya Mola wao Mlezi na madhila katika maisha ya duniani. Na kama hivyo ndivyo tunavyowalipa wazushi



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 194

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Hakika, wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allah ni waja mfano wenu (ni waja kama nyinyi). Basi waombeni wakuitikieni, ikiwa nyinyi ni wakweli



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 197

وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَكُمۡ وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ

Na wale mnaowaomba badala yake hawawezi kukunusuruni wala wao wenyewe hawawezi kujinusuru



Sura: AL-AARAAF 

Aya : 198

وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَسۡمَعُواْۖ وَتَرَىٰهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ وَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ

Na kama mtawaita wafuate muongozo (wa Allah) hawasikii, na utawaona wanakukodolea macho na ilhali hawaoni



Sura: YUNUS 

Aya : 18

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَـٰٓؤُلَآءِ شُفَعَـٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na wanaabudu badala ya Allah vitu visivyo wadhuru wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allah”. Sema: Hivi mnamwambia Allah mambo asiyoyajua mbinguni na ardhini[1]? Utakasifu ni wake (Allah) na ametukuka na yuko mbali na vyote wanavyovishirikisha naye


1- - Allah hapa anamuamuru Mtume wake Muhammad, Allah amshushie rehema na amani, awaambie hawa makafiri washirikishaji kwamba: Allah Mtukufu ndiye mmiliki wa mbingu na ardhi hakifichikani kwake chochote humo. Hivi wanamfundisha na kumueleza vitu visivyokuwepo humo.


Sura: YUNUS 

Aya : 69

قُلۡ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ

Sema: Hakika, wale wanaomzushia Allah uwongo, hawafaulu



Sura: YUNUS 

Aya : 70

مَتَٰعٞ فِي ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ ٱلۡعَذَابَ ٱلشَّدِيدَ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ

Ni starehe (ndogo) tu duniani, kisha marejeo yao ni kwetu tu, kisha tutawaonjesha adhabu kali, kwa sababu ya ukafiri waliokuwa wakiufanya



Sura: HUUD 

Aya : 101

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ

Na sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamezidhulumu nafsi zao. Na haikuwafaa chochote Miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Allah ilipokuja amri ya Mola wako mlezi. Na hiyo Miungu haikuwazidishia kitu isipokuwa maangamizi tu



Sura: AR-RA’D 

Aya : 17

أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَسَالَتۡ أَوۡدِيَةُۢ بِقَدَرِهَا فَٱحۡتَمَلَ ٱلسَّيۡلُ زَبَدٗا رَّابِيٗاۖ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيۡهِ فِي ٱلنَّارِ ٱبۡتِغَآءَ حِلۡيَةٍ أَوۡ مَتَٰعٖ زَبَدٞ مِّثۡلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ وَٱلۡبَٰطِلَۚ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذۡهَبُ جُفَآءٗۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمۡكُثُ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ

(Allah) Ameteremsha maji kutoka mawinguni. Na mabonde yakatiririsha maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyokusanyika juu yake. Na baadhi ya (madini) wanayo yayeyusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile (wakati wa kuyayusha). Namna hiyo ndivyo Allah anavyopiga mifano ya haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu. Ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Allah anavyopiga mifano



Sura: ANNAHLI 

Aya : 105

إِنَّمَا يَفۡتَرِي ٱلۡكَذِبَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ

Hakika sivingine wanaozua uongo ni wale tu wasioziamini Aya za Allah, na hao ndio waongo (hasa)



Sura: ANNAHLI 

Aya : 116

وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ

Na msiseme (enyi washirikina), kwa uongo ambao usemwao na ndimi zenu kuwa, hii halali (kwanini Allah ameiharamisha) na hii haramu (kwanini ameihalalisha), ili kumzulia Allah uongo. Hakika wale wamzuliao Allah uongo hawatafaulu[1]


1- - Katika Aya hii Allah anabainisha kuwa uhalali wa kitu na uharamu hatokani na utashi wa mtu ama watu, bali ni msingi uliyowekwa na Allah mwenyewe kwa viumbe wake, hivyo anawakemea washirikishaji na Makafiri kwa ujumla, wasihalalishe au kuharamisha kitu kwa utashi wa nafsi zao. Kilicho halali ni kile alicha halalisha Allah, na haramu ni kile alicho kiharamisha Allah.


Sura: AL-ISRAA 

Aya : 56

قُلِ ٱدۡعُواْ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمۡلِكُونَ كَشۡفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمۡ وَلَا تَحۡوِيلًا

Sema: Waombeni hao mnao wadaia badala yake Yeye. Hawawezi kukuondoleeni madhara, wala kuyaweka pengine



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 57

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ يَبۡتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلۡوَسِيلَةَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ وَيَرۡجُونَ رَحۡمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحۡذُورٗا

Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo



Sura: AL-ISRAA 

Aya : 67

وَإِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فِي ٱلۡبَحۡرِ ضَلَّ مَن تَدۡعُونَ إِلَّآ إِيَّاهُۖ فَلَمَّا نَجَّىٰكُمۡ إِلَى ٱلۡبَرِّ أَعۡرَضۡتُمۡۚ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ كَفُورًا

Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na anapo kuvusheni mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanaadamu ni mwingi wa kukanusha