Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 87

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَقَفَّيۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ بِٱلرُّسُلِۖ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ أَفَكُلَّمَا جَآءَكُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُكُمُ ٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡ فَفَرِيقٗا كَذَّبۡتُمۡ وَفَرِيقٗا تَقۡتُلُونَ

Na kwa hakika tulimpa Musa Kitabu, na tukafuatishia baada yake kwa kupeleka Mitume, na tukampa Isa Mwana wa Mariamu miujiza iliyo wazi na tukampa nguvu kwa Roho Mtakatifu (Jibrili). Basi je, kila Mtume akikuleteeni yale yasiyopendwa na nafsi zenu mnafanya kiburi? (Mitume) Wengine mliwapinga na wengine mliwaua



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 97

قُلۡ مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّـجِبۡرِيلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلۡبِكَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Sema: Mwenye kuwa adui wa Jibrili, basi (ajue kuwa) yeye ndiye aliyeuteremsha Wahyi (Qur’an) moyoni mwako kwa idhini ya Allah, unaosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake na ni muongozo na bishara kwa waumini



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 98

مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّلَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبۡرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوّٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ

Mwenye kuwa adui wa Allah na Malaika wake na Mitume wake na Jibrilina Mikaili, basi hakika, Allah ni adui wa makafiri wote



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 253

۞تِلۡكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلۡنَا بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۘ مِّنۡهُم مَّن كَلَّمَ ٱللَّهُۖ وَرَفَعَ بَعۡضَهُمۡ دَرَجَٰتٖۚ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلَ ٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ وَلَٰكِنِ ٱخۡتَلَفُواْ فَمِنۡهُم مَّنۡ ءَامَنَ وَمِنۡهُم مَّن كَفَرَۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلُواْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفۡعَلُ مَا يُرِيدُ

Hao Mitume baadhi yao tumewatukuza zaidi kuliko wengine. Katika wao wapo ambao Allah alisema nao, na baadhi yao amewatukuza daraja mbalimbali. Na Isa mwana wa Mariamu tukampa hoja zilizo wazi, na tulimpa nguvu kwa Roho Takatifu. Na kama Allah angetaka, wasingelipigana waliokuja baada yao, baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, na lakini walihitilafiana. Basi wapo miongoni mwao walioamini, na wapo miongoni mwao waliokufuru. Na kama Allah angelitaka, wasingelipigana na lakini Allah hufanya ayatakayo



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 110

إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱذۡكُرۡ نِعۡمَتِي عَلَيۡكَ وَعَلَىٰ وَٰلِدَتِكَ إِذۡ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِ تُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗاۖ وَإِذۡ عَلَّمۡتُكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَۖ وَإِذۡ تَخۡلُقُ مِنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِ بِإِذۡنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِيۖ وَتُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ تُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ كَفَفۡتُ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ عَنكَ إِذۡ جِئۡتَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

(kumbuka) Pale Allah aliposema: Ewe Issa bin Mariamu, kumbuka neema yangu kwako na kwa mama yako, nilipokutia nguvu kwa Roho Mtakatifu (Jibrili), ukazungumza na watu katika utoto na ukiwa mtumzima. Na (kumbuka) nilivyokufundisha kitabu na hekima na Taurati na Injili, na wakati unaunda kutokana na udongo mfano wa ndege kwa idhini yangu, kisha unapuliza katika mfano huo na wakawa ndege kwa idhini yangu, na (kumbuka) ulipowaponyesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini yangu, na (kumbuka) wakati unawafufua wafu kwa idhini yangu. Na (kumbuka) nilipowazuia Wana wa Israili wasikudhuru ulipowaendea na hoja zilizo wazi, wakasema waliokufuru miongoni mwao (kwamba): Haya (aliyoyaleta Issa) si lolote isipokuwa tu ni uchawi mtupu!



Sura: ANNAHLI 

Aya : 102

قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ

Sema: Ameiteremsha Roho mtakatifu (Jibrili) kutoka kwa Mola wako mlezi kwa haki kabisa, ili kuwaimarisha wale walioamini, na kuwa mwongozo na habari njema kwa Waislamu



Sura: ASH-SHUARAA 

Aya : 193

نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلۡأَمِينُ

Ameuteremsha Roho mua-minifu,(jibril)



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 4

إِن تَتُوبَآ إِلَى ٱللَّهِ فَقَدۡ صَغَتۡ قُلُوبُكُمَاۖ وَإِن تَظَٰهَرَا عَلَيۡهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ مَوۡلَىٰهُ وَجِبۡرِيلُ وَصَٰلِحُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ

Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (yanayomchukiza Mtume). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake kipenzi chake, na Jibrili na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 12

وَمَرۡيَمَ ٱبۡنَتَ عِمۡرَٰنَ ٱلَّتِيٓ أَحۡصَنَتۡ فَرۡجَهَا فَنَفَخۡنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتۡ بِكَلِمَٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِۦ وَكَانَتۡ مِنَ ٱلۡقَٰنِتِينَ

Na Mariamu binti wa ‘Imrani ambaye amehifadhi tupu yake (aliye linda ubikira wake), Tukampulizia humo (katika nguo yake) kupitia kwa Roho Wetu (Jibrili), na akasadikisha Maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa watiifu na wanyenyekevu



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 4

تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ

Malaika na Roho (Jibrili) wanapanda kwenda kwake katika siku ambayo makadirio yake ni miaka hamsini elfu



Sura: ANNABAI 

Aya : 38

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا

Siku atakayosimama Roho (Jibrili) na Malaika hali ya kujipanga safu; Hawatasema ila aliye mruhusu Mwingi wa rehema, na atasema yaliyo sawa tu



Sura: ATTAK-WIIR 

Aya : 19

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Hakika hii (Qurani) bila shaka ni kauli (ameifikisha) Mjumbe mtukufu (Jibrili)



Sura: ATTAK-WIIR 

Aya : 20

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٖ

Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allah) Anayemiliki ‘Arsh. [Kiti cha Enzi]



Sura: ATTAK-WIIR 

Aya : 21

مُّطَاعٖ ثَمَّ أَمِينٖ

Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni)



Sura: AL-QADRI 

Aya : 4

تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ

Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo