Sura: ASSWAFF 

Aya : 2

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفۡعَلُونَ

Enyi mlioamini, kwanini mnasema msiyoyafanya?



Sura: ASSWAFF 

Aya : 3

كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ أَن تَقُولُواْ مَا لَا تَفۡعَلُونَ

Imekuwa chukizo kubwa mno mbele ya Allah kwamba mnasema msiyoyafanya



Sura: ASSWAFF 

Aya : 4

إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِهِۦ صَفّٗا كَأَنَّهُم بُنۡيَٰنٞ مَّرۡصُوصٞ

Kwa hakika, Allah anawapenda wanaopigana katika njia yake wakiwa safu (moja) kama jengo liliokamatana



Sura: ASSWAFF 

Aya : 5

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ لِمَ تُؤۡذُونَنِي وَقَد تَّعۡلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡۖ فَلَمَّا زَاغُوٓاْ أَزَاغَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Na (kumbuka Musa) Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu: Kwanini mnaniudhi, na ilhali mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Allah niliyetumwa kwenu? Basi walipo potoka, Allah aliziachia nyoyo zao zipotoke. Na Allah hawaongozi watu waovu



Sura: ASSWAFF 

Aya : 6

وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na (kumbuka Mtume) Isa, Mwana wa Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili: Hakika, mimi ni Mtume wa Allah kwenu, nikithibitisha Taurati iliyokuwepo kabla yangu, na nikitoa bishara (habari njema) ya Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad. Lakini (Mtume huyo) alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhahiri



Sura: ASSWAFF 

Aya : 7

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُوَ يُدۡعَىٰٓ إِلَى ٱلۡإِسۡلَٰمِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anaye mzulia Allah uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Allah hawaongoi watu madhaalimu



Sura: ASSWAFF 

Aya : 8

يُرِيدُونَ لِيُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَٱللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Wanataka kuizima nuru ya Allah kwa vinywa vyao. Na Allah atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia



Sura: ASSWAFF 

Aya : 9

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُشۡرِكُونَ

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia



Sura: ASSWAFF 

Aya : 10

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ تِجَٰرَةٖ تُنجِيكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ

Enyi mlioamini! Nikujulisheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu (iumizayo)?



Sura: ASSWAFF 

Aya : 11

تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Muaminini Allah na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Allah kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua



Sura: ASSWAFF 

Aya : 12

يَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡ وَيُدۡخِلۡكُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّـٰتِ عَدۡنٖۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa



Sura: ASSWAFF 

Aya : 13

وَأُخۡرَىٰ تُحِبُّونَهَاۖ نَصۡرٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتۡحٞ قَرِيبٞۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na kingine mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Allah, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!



Sura: ASSWAFF 

Aya : 14

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُوٓاْ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ لِلۡحَوَارِيِّـۧنَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٞ مِّنۢ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٞۖ فَأَيَّدۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَىٰ عَدُوِّهِمۡ فَأَصۡبَحُواْ ظَٰهِرِينَ

Enyi walioamini! Kuweni wenye kuinusuru (Dini ya) Allah kama alivyosema ‘Isa mwana wa Maryam kwa wafuasi wake (watiifu): Na ni wanusuruji wangu kwa ajili ya Allah? Wafuasi wake wakasema: Sisi ni wenye kuinusuru (Dini ya) Allah, Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israail na likakufuru kundi jingine. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 1

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡمَلِكِ ٱلۡقُدُّوسِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Vinamtakasa Allah (viumbe) vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Mfalme, Mtukufu, Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 2

هُوَ ٱلَّذِي بَعَثَ فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Yeye (Allah) ndiye aliye mpeleka Mtume kwa watu wasiojua kusoma wala kuandika, awasomee Aya zake na awatakase na awafunze Kitabu na hekima, japokuwa kabla ya haya walikuwa katika upotevu ulio wazi kabisa



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 3

وَءَاخَرِينَ مِنۡهُمۡ لَمَّا يَلۡحَقُواْ بِهِمۡۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na wengineo ambao bado hawajakutana nao. Naye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 4

ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Hiyo ni fadhila ya Allah anayo mpa amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kubwa



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 5

مَثَلُ ٱلَّذِينَ حُمِّلُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ ثُمَّ لَمۡ يَحۡمِلُوهَا كَمَثَلِ ٱلۡحِمَارِ يَحۡمِلُ أَسۡفَارَۢاۚ بِئۡسَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za Allah, na Allah hawaongoi watu madhaalimu



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 6

قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ هَادُوٓاْ إِن زَعَمۡتُمۡ أَنَّكُمۡ أَوۡلِيَآءُ لِلَّهِ مِن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Enyi Mayahudi! Mkidai kuwa nyinyi ni vipenzi vya Allah pasina watu wengine, basi tamaneni kufa, mkiwa ni wasemao kweli



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 7

وَلَا يَتَمَنَّوۡنَهُۥٓ أَبَدَۢا بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ

Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza mikono yao. Na Allah anawajua walio dhulumu



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 8

قُلۡ إِنَّ ٱلۡمَوۡتَ ٱلَّذِي تَفِرُّونَ مِنۡهُ فَإِنَّهُۥ مُلَٰقِيكُمۡۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo atakwambieni mliyokuwa mkiyatenda



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 9

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوۡمِ ٱلۡجُمُعَةِ فَٱسۡعَوۡاْ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَذَرُواْ ٱلۡبَيۡعَۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Sala siku ya Ijumaa, kimbilieni kumcha Allah na acheni kuuza na kununua. Hilo ni kheri kwenu mkiwa mnajua



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 10

فَإِذَا قُضِيَتِ ٱلصَّلَوٰةُ فَٱنتَشِرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَٱبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Na inapomalizika Swalaah, tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni katika fadhila za Allah, na mcheni Allah sana ili mpate kufaulu



Sura: AL-JUMUA 

Aya : 11

وَإِذَا رَأَوۡاْ تِجَٰرَةً أَوۡ لَهۡوًا ٱنفَضُّوٓاْ إِلَيۡهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمٗاۚ قُلۡ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ مِّنَ ٱللَّهۡوِ وَمِنَ ٱلتِّجَٰرَةِۚ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلرَّـٰزِقِينَ

Na wanapoona biashara au pumbao (mambo ya upuuzi) wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Allah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allah ni Mbora wa wenye kuruzuku



Sura: ALMUNAAFIQUUN 

Aya : 1

إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ قَالُواْ نَشۡهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُۥ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَكَٰذِبُونَ

Watakapokujia wanafiki wanasema: Tunashuhudia kwamba wewe bila ya shaka yoyote ni Mtume wa Allah. Na Allah Anajua kuwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Allah anashuhudia kuwa kwa hakika kabisa wanafiki ni waongo



Sura: ALMUNAAFIQUUN 

Aya : 2

ٱتَّخَذُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ جُنَّةٗ فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Wamefanya viapo vyao ni ngao, hivyo wakazuia (watu wasiifuate) njia ya Allah. Hakika, ni uovu mno waliokuwa wakiufanya



Sura: ALMUNAAFIQUUN 

Aya : 3

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ

Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa (chapa) ya muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote



Sura: ALMUNAAFIQUUN 

Aya : 4

۞وَإِذَا رَأَيۡتَهُمۡ تُعۡجِبُكَ أَجۡسَامُهُمۡۖ وَإِن يَقُولُواْ تَسۡمَعۡ لِقَوۡلِهِمۡۖ كَأَنَّهُمۡ خُشُبٞ مُّسَنَّدَةٞۖ يَحۡسَبُونَ كُلَّ صَيۡحَةٍ عَلَيۡهِمۡۚ هُمُ ٱلۡعَدُوُّ فَٱحۡذَرۡهُمۡۚ قَٰتَلَهُمُ ٱللَّهُۖ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ

Na ukiwaona miili yao inakupendeza kwa uzuri wao, na wakizungumza unavutika kuwasikiliza kwa utamu wa maneno. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa (hayana uhai wowote wa Imani). Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Allah awaangamizie mbali! Namna gani wanavyoghilibiwa (na kuiacha haki)?



Sura: ALMUNAAFIQUUN 

Aya : 5

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ يَسۡتَغۡفِرۡ لَكُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوۡاْ رُءُوسَهُمۡ وَرَأَيۡتَهُمۡ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Na wanapo ambiwa: Njooni ili Mtume wa Allah akuombeeni maghfira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi



Sura: ALMUNAAFIQUUN 

Aya : 6

سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ أَسۡتَغۡفَرۡتَ لَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ لَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Ni sawasawa juu yao, ukiwaombea maghfirah au usiwaombee, Allah Hatowaghufuria kamwe. Hakika Allah Haongoi watu mafasiki