Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 1

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu



Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 2

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Kila sifa njema ni ya Allah, Mola wa walimwengu wote



Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 3

ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Mwingi wa Rehema, Mwenye-Kurehemu



Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 4

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Mmiliki wa Siku ya Malipo



Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 5

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ

Wewe tu ndiye tunae kuabudu na wewe tu ndie tunae kuomba msaada



Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 6

ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ

Tuongoze kwenye njia ilio nyooka



Sura: AL-FAATIHA 

Aya : 7

صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ

Njia ya ambao umewaneemesha, na sio yawalio kasirikiwa na sio ya waliopotea[1]


1- - Walioneemeshwa wametajwa katika Sura AnNisaa (4), Aya ya 69. Hapa Aya inaashiria utukufu wa Swahaba wa kiongozwana Abubakar, Umar, Uthman na Ali (Allah awawieradhi) kwasababu wao ni miongoni mwa walioneemeshwa na ambao tunatakiwa kufuata njia yao. Waliokasirikiwa wametajwa kuanzia Aya ya 75 mpaka Aya ya 90 ya Sura Albaqara, na waliopotea wametajwa katika Aya ya 77 ya Sura Almaida (5).


Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 1

الٓمٓ

Alif Laam Miim[1]


1- - Allah ndiye ajuwaye zaidi madhumuni ya herufi hizi.


Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 2

ذَٰلِكَ ٱلۡكِتَٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدٗى لِّلۡمُتَّقِينَ

Kitabu hiki hakina shaka. Ni muongozo kwa Wacha Mungu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 3

ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

Ambao wanaamini Ghaibu na wanasimamisha swala na baadhi ya tulivyowapa wanatoa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 4

وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ وَبِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ

Na ambao wanaamini yale tuliyoyateremsha kwako na yale tuliyoyateremsha kabla yako, na ambao wanaamini Akhera



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 5

أُوْلَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدٗى مِّن رَّبِّهِمۡۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Hao wako juu ya muongozo utokao kwa Mola wao, na hao tu ndio waliofaulu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 6

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hakika, waliokufuru, ni sawa kwao umewahadharisha au hukuwahadharisha; hawaamini



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 7

خَتَمَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَعَلَىٰ سَمۡعِهِمۡۖ وَعَلَىٰٓ أَبۡصَٰرِهِمۡ غِشَٰوَةٞۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Allah amefunga nyoyo zao na usikivu wao, na katika uonaji wao kuna kifuniko, na watastahiki adhabu kubwa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 8

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ

Na miongoni mwa watu wapo wanaosema[1] kuwa: “Tumemuamini Allah na Siku ya Mwisho” na[2] sio waumini (wa kweli)


1- - Kwa maneno tu.


2- - Ukweli ni kwamba…


Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 9

يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Wanamhadaa Allah na wale walioamini. Na hawahadai isipokuwa nafsi zao tu na wao hawatambui



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 10

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ

Ndani ya nyoyo zao kuna ugonjwa, na Allah akawaongezea ugonjwa. Na wanastahiki adhabu kali kwa uongo waliokuwa wanaufanya



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 11

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ قَالُوٓاْ إِنَّمَا نَحۡنُ مُصۡلِحُونَ

Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ardhini wanasema: Hapana, bali sisi niwafanyaji mazuri



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 12

أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡمُفۡسِدُونَ وَلَٰكِن لَّا يَشۡعُرُونَ

Elewa! Kwa yakini, wao ndio waharibifu hasa na lakini hawatambui



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 13

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ كَمَآ ءَامَنَ ٱلنَّاسُ قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ كَمَآ ءَامَنَ ٱلسُّفَهَآءُۗ أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلسُّفَهَآءُ وَلَٰكِن لَّا يَعۡلَمُونَ

Na wanapoambiwa: Kuweni wenye kuamini kama walivyoamini watu, wanasema: Ah! Hivi tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Elewa! Wao ndio wapumbavu hasa na lakini hawajui



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 14

وَإِذَا لَقُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَوۡاْ إِلَىٰ شَيَٰطِينِهِمۡ قَالُوٓاْ إِنَّا مَعَكُمۡ إِنَّمَا نَحۡنُ مُسۡتَهۡزِءُونَ

Na wanapokutana na walioamini wanasema: Tumeamini. Na wanapokuwa faragha na mashetani wao wanasema: Sisi tuko pamoja nanyi, tunachokifanya sisi tunacheza shere tu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 15

ٱللَّهُ يَسۡتَهۡزِئُ بِهِمۡ وَيَمُدُّهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Allah anawacheza shere wao, na anawapa muda zaidi katika kupotoka kwao huku wakiwa wanatangatanga



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 16

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَٰرَتُهُمۡ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Hao ndio walioununua upotevu kwa uongofu. Biashara yao haikuleta faida, na hawakuwa waongofu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 17

مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ

Mfano wao ni kama mfano wa mtu aliyewasha moto. Kila moto ulipomuangazia maeneo yanayomzunguka, Allah akaondoa mwanga wao na kuwaacha katika kiza kinene; hawaoni



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 18

صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَرۡجِعُونَ

Ni viziwi, mabubu, vipofu. Kwa sababu hiyo, hawarudi



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 19

أَوۡ كَصَيِّبٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَٰتٞ وَرَعۡدٞ وَبَرۡقٞ يَجۡعَلُونَ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِم مِّنَ ٱلصَّوَٰعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ

Au ni kama mvua iteremkayo kwa kasi kutoka mawinguni, ndani yake mna kiza kinene na radi na umeme wanaweka vidole vyao masikioni mwao kutokana na radi kwa kuhadhari kifo. Na Allah amewazunguka makafiri wote



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 20

يَكَادُ ٱلۡبَرۡقُ يَخۡطَفُ أَبۡصَٰرَهُمۡۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوۡاْ فِيهِ وَإِذَآ أَظۡلَمَ عَلَيۡهِمۡ قَامُواْۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Umeme unakaribia kupofoa macho yao. Kila unapowaangazia wanatembea katika mwanga huo, na pale unapowazimikia wanasimama. Na kama Allah angelitaka basi, kwa yakini kabisa, angeondoa kusikia kwao na macho yao. Hakika, Allah ni muweza wa kila kitu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 21

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Enyi watu, muabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na (ameumba) waliokuwepo kabla yenu ili muwe Wacha Mungu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 22

ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فِرَٰشٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ فَلَا تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Ambaye amekuumbieni ardhi ikiwa imetandazwa, na mbingu ikiwa sakafu na ameteremsha kutoka mawinguni maji (mvua), akatoa kwa maji hayo riziki zenu kutoka kwenye matunda. Basi msimfanyie Allah washirika ilihali mnajua (kuwa Allah hana mshirika)



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 23

وَإِن كُنتُمۡ فِي رَيۡبٖ مِّمَّا نَزَّلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّن مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na ikiwa mna shaka na kile tulichomteremshia mja wetu, basi leteni Sura (moja tu) iliyo mithili yake, na waleteni mashahidi wenu badala ya Allah ikiwa nyinyi ni wa kweli